Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
katika kivuli katika taratibu za kiibada katika picha (taswira)
katika mwili halisi katika uhalisi mhusika/mtu halisi
Waebrani 10:7
kama aliyetabiriwa katika unabii katika Kristofania (kuonekana kabla ya umwilisho)
kama utimilifu katika historia katika mwili (umwilisho)
Luka 24:27, 44 Yohana 5:39
Uhusiano kati ya maagano haya unaweza kugawanywa kwa ujumla katika madaraja matatu yanayolingana na njia pana ambazo Kristo anapatikana katika Agano la Kale. Katika kila kisa milinganisho miwili ya kwanza iliyoorodheshwa hapo juu takriban inafanana, lakini kwa vile ina maana tofauti imeorodheshwa tofauti ili kuendeleza ufafanuzi wa ulinganisho kati ya maagano. KRISTO: KUFICHWA KATIKA AGANO LA KALE NA KUFUNULIWA KATIKA AGANO JIPYA Augustine alisema: “Jipya limefichwa ndani ya la Kale, na la Kale limefunuliwa ndani ya Jipya.” Au, kama mtu mwingine alivyosema, Jipya limefunikwa katika lile la Kale, na la Kale limefunuliwa katika Jipya. Sasa, hakuna tatizo katika kumwona Kristo ndani ya Agano Jipya: Injili zinamtambulisha kama Nabii kwa watu wake; Matendo na Nyaraka zinamfunua kama Kuhani kwa watu wake, katika mkono wa kuume wa Mungu; na Ufunuo unatabiri kwamba atakuwa Mfalme juu ya watu wake wote.
60
Made with FlippingBook Digital Publishing Software