Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
SURA YA 3 | KRISTO KATIKA MAAGANO YOTE MAWILI
KWA KUWA KRISTO NDIYE MADA KUU YA AGANO LA KALE KWA UJUMLA WAKE, kama ambavyo Yeye Mwenyewe alithibitisha mara tano (Mt. 5:17; Lk. 24:27, 44; Yoh. 5:39; Ebr. 10:7), basi uhusiano kati ya A.K na A.J umeunganishwa na nafsi ya Kristo na hauwezi kutenganishwa naye. Uchunguzi wa uhusiano huo ndiyo mada ya sura hii. Ikiwa Kristo ndiye “kiunganishi” cha kitabu cha Maandiko, basi itakuwa vigumu kuielewa Biblia nzima bila ujuzi wa uhusiano wa sehemu zake mbili za msingi. Sasa basi, maagano haya mawili yanahusiana vipi? Uhusiano wa Jumla kati ya Agano la Kale na Jipya Uhusiano wa jumla kati ya A.K na A.J ni ule wa kutegemeana. Agano la Kale halijakamilika bila Jipya. Kile ambacho Agano la Kale lilitayarisha, Agano Jipya linatimiza katika Kristo. Kristo ndiye tarajio la lile ya Kale na utimilifu wa Jipya. Kwa maana kile kilichoanzishwa katika Agano la Kale kinakamilishwa katika Agano Jipya, na kweli ya Kristo katika Agano Jipya haiwezi kueleweka mbali na msingi uliowekwa kwa ajili yake katika Agano la Kale. Uhusiano huu wa kutegemeana unaweza kuelezewa kama ifuatavyo: Kristo katika Maagano Yote Mawili
Matarajio katika Agano la Kale limefichwa limejumuishwa sheria
Utimilifu katika Agano Jipya limefunuliwa limefafanuliwa utimilifu wake
Katika
Mathayo 5:17
59
Made with FlippingBook Digital Publishing Software