Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
la Kale. Baada ya kuchunguza vifungu hivi, tumehitimisha kwamba kuna namna au njia nne ambazo Kristo ni utimilifu wa Agano la Kale. Yeye ni utimilifu wa: • Unabii wa Kimasihi wa Agano la Kale (kama inavyoonyeshwa katika Luka na Matendo) • Ukuhani wa Walawi wa Agano la Kale (kama inavyoonyeshwa katika Waebrania) • Sheria za maadili za Agano la Kale (kama inavyoonyeshwa katika Mathayo) • Ahadi za wokovu za Agano la Kale (kama inavyoonyeshwa katika Yohana). Kila moja ya maoni haya yanawasilisha kipengele tofauti cha huduma ya Kristo, mtawalia; • Unabii wa Kimasihi unamwona kama Masihi na Mfalme; • Ukuhani wa Walawi, kama Kuhani na Dhabihu; • Sheria za maadili, kama Nabii na Mwalimu; • Ahadi za wokovu, kama Bwana na Mwokozi. Tunaweza kuhitimisha, basi, kwamba kuna njia kadhaa halali za kulitafsiri Agano la Kale katika msingi wa Kristo, lakini hakuna njia halali za kulitafsiri Agano la Kale nje ya msingi wa Kristo. Yesu alisema, “Kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?” (Yh 5:46-47).
58
Made with FlippingBook Digital Publishing Software