Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
7. Yuda angepotea (Yh 17:12, taz. Zab. 41:9) 8. Mtu mwingine angechukua nafasi ya Yuda (Mdo 1:20, taz. Zab. 69:25; 109:8) Utimilifu wa Picha za Kimasihi Kando na “kanuni” za Kimasihi, ambazo zinatumika kwa habari ya Kristo katika Agano Jipya, kuna vifungu vingine kama hivyo na ambavyo waandishi wa Agano Jipya hawakuwa na nafasi ya kuvitumia (ingawa wangeweza kuvitumia kihalali kuhusiana na ya Kristo). Hizi “picha za Kimasihi” hazikukusudiwa kuwa utabiri, lakini ziliakisi kwa namna inayofaa kile ambacho Masihi alifanya. Ni mafumbo yaliyochukuliwa kutokana na maisha ya watu wa taifa la Kimasihi ambayo yanaweza kutumika kwa ukamilifu zaidi kwa kuyahusianisha na Masihi mwenyewe. Kwa mfano, kuna utimilifu au ukamilifu wa picha zifuatazo katika Kristo: • Kumwelekezea shavu lake yule ampigaye (Omb. 3:30, taz. Mt. 27:30). • Jua likawa giza wakati wa adhuhuri (Amo 8:9, taz. Mt. 27:45) • Israeli wakiomboleza kwa ajili ya mwana wa pekee (Amo 8:10, taz. Lk 23:28) Sehemu kubwa ya dhana zilizotiwa chumvi katika elimu ya Kimasihi inaweza kuondolewa “chumvi” na ikafaa kuwekwa katika kundi hili na hivyo kutambuliwa kama utimilifu au ukamilifu wa “picha” za Kristo, badala ya kuchukuliwa kama utabiri halisi kumhusu Yeye. Hata hivyo, kunapaswa kuwa na mipaka fulani ya makusudi kwa mafumbo ya Kimasihi yanayotumiwa kumhusu Kristo. Labda kanuni inapaswa kuwa: kifungu chochote cha Agano la Kale kinaweza kuhusianishwa na Kristo, ingawa • Kumpa siki Kristo msalabani (Zab. 69:21, taz. Mt. 27:48) • Hekima kufanyika mtu (Mit. 8, rej 1 Kor. 1:30; Kol. 2:3)
73
Made with FlippingBook Digital Publishing Software