Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
waandishi wa Agano Jipya hawakukinukuu, kwa sharti kwamba kinatoa mfano wa kitu fulani katika maisha ya watu wa Kimasihi ambacho kinapata ulinganifu halisi na ukweli juu ya Kristo unaopatikana mahali fulani katika Biblia. Au, kwa maneno mengine, ikiwa kifungu na kanuni inayohusika ndani yake ni sawa na ile iliyotajwa na waandishi wa Agano Jipya, basi kinaweza kuhusishwa kwa uhalali na Kristo. Labda ugumu wa kubainisha ni aina gani ya unabii wa kifungu fulani unaweza kutambuliwa zaidi ikiwa itakumbukwa kwamba manabii wenyewe waliyachunguza maandiko yao ili kupata “ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho wa Kristo aliyekuwa ndani yao” (1 Pet 1:11). Kwa maneno mengine, ukweli juu ya Kristo mara nyingi ulidokezwa tu katika maandiko ya kinabii na haukuwekwa wazi hadi kipindi cha Agano Jipya kilipokuja. Yesu alitoa mfano wa hili aliponukuu Isaya 61:1-2 na kusimama katikati ya mstari huo, akiwatangazia watu kwamba “leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu” (Lk 4:21). Maneno yanayofuata, ambayo Yesu hakuyasoma yanasema, “…na siku ya kisasi cha Mungu wetu…” Maneno haya yalirejelea ujio wa pili wa Kristo, na hivyo hakuyanukuu kama yaliyotimia katika kuja kwake mara ya kwanza . Bonde refu la muda ambao ungepita kati ya vilele hivi viwili vya milima ya ukweli kuhusu ujio wa Kristo (yaani ujio wa kwanza na ule wa pili) halikufunuliwa waziwazi katika Agano la Kale. Matokeo yake, ukweli mwingi wa kinabii uliofumbwa katika Agano la Kale haukufunuliwa hadi kipindi cha Agano Jipya. Tangu Kristofania hadi Umwilisho Hatimaye, kuna uhusiano mwingine kati ya Agano la Kale na Agano Jipya juu ya kiwango cha Masihi: katika Agano la Kale kulikuwa na kuonekana kwa Kristo kabla ya kuzaliwa katika mwili, na katika Agano Jipya kuna kufanyika mwili kwa Kristo. Kutokea kwa Kristo katika Agano la Kale (Kristofania) tayari kumejadiliwa (katika sura ya 2) katika kipengele
74
Made with FlippingBook Digital Publishing Software