Kristo: Mada Kuu Ya Biblia

cha “malaika wa BWANA.” Hapa itabainishwa kwa ufupi jinsi kufanyika mwili kwa Kristo katika Agano Jipya kunahusiana na kunachukua nafasi ya matukio haya ya Kristofania katika Agano la Kale. Kwa jambo moja, kuonekana huku katika Agano la Kale kulikuwa kwa mara chache, hapa na pale (Mwa. 16, 22, 31, 48; Kut. 3; Yos. 5; Amu 2, 6, 13; 2 Fal 1, 19), ambapo katika Agano Jipya uwepo wa Kristo ni wa daima . Kwa kuongezea, kuonekana huku [au Kristofania] kulikuwa kwa muda tu, lakini umwilisho wake ni wa kudumu . Malaika wa Bwana alionekana mara kadha wa kadha kabla ya kuzaliwa kwa Kristo na hakuonekana tena kabisa baada ya Kristo kuzaliwa. Malaika wa Bwana (Gabrieli) alimtokea Yusufu (Mat.1:20); malaika wa Bwana alizungumza na Filipo (Mdo 8:26); na malaika wa Bwana akamtoa Petro gerezani (Mdo 12:7), lakini si malaika wa Bwana yule wa A.K. Zaidi ya hayo, “malaika wa Bwana” wa Agano Jipya hakuruhusu kuabudiwa, jambo ambalo ni tofauti na “malaika wa BWANA” katika Agano la Kale (rej. Ufu. 22:8-9), ambapo “malaika wa Bwana” katika Agano la Kale alidai ibada (rej. Kut. 3:5; Yos. 5:15). Lakini Kristo alipochukua mwili, alifanyika Mungu-Mtu milele. Yohana anasema: “Naye Neno [Kristo] alifanyika mwili, akakaa kwetu” (1:14). Waebrania anasema: “Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye [Kristo] vivyo hivyo alishiriki yayo hayo” (2:14). Ufufuo wa Kristo katika wafu ulikuwa wa kimwili (rej. Lk 24:39), kama kulivyokuwa kupaa kwake mbinguni (Mdo 1:9-11). Na katika kikao chake cha sasa katika mkono wa kuume wa Mungu, Kristo angali amehifadhi muungano na mwili wake. Wakolosai 2:9 inasema juu ya Kristo aliyepaa, “Maana katika yeye unakaa [wakati uliopo] utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili .” Na, kulingana na unabii, Kristo atarudi duniani akiwa na mwili na kutawala milele (Mdo 1:11, taz. Zek. 14:4, n.k.). Paulo aliandika juu ya Kristo kwamba “alidhihirishwa katika mwili ” (1 Tim. 3:16), na Yohana aliona kuwa ni uzushi kuukana ubinadamu wa Kristo, akasema:

75

Made with FlippingBook Digital Publishing Software