Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
“Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu. Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu” (1 Yh 4:2-3). Ni lazima kuzingatia kwamba kupata mwili kwa Kristo hakukuwa tu “kuonekana” kwa mwili; ilikuwa ni “udhihirisho” katika mwili. Kristo hakuwa na “umbo” tu la mwili, bali alikuwa mwili kwa namna ile ile kama sisi tulivyo, “bila kufanya dhambi” (Ebr. 4:15). Ni katika maana hii ya mwisho tu ambapo ubinadamu wa Kristo unasemwa kuwa “ mfano wa wanadamu” (Flp. 2:7). Asili ya Kristo ya kibinadamu ilikuwa tofauti na yetu kwa kuwa tu haikuwa na dhambi; lakini katika vipengele vingine ilikuwa sawa kabisa na yetu (Warumi 8:3). Sasa aina hii ya umwilisho inapita matukio ya Kristofania ya Agano la Kale sio tu kwa kuwa ni udhihirisho endelevu, wa kudumu na wa kweli wa kibinadamu lakini kwa kuwa pia ni bora kuliko njia za Agano la Kale za ufunuo. Katika Agano la Kale Mungu alijidhihirisha katika sheria na taratibu , lakini katika Agano Jipya anafunuliwa katika maisha ya Kristo. Yesu alitangaza, “Aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yh 14:9). Katika Agano la Kale Mungu alijidhihirisha kupitia kauli (neno) , lakini katika Kristo ufunuo wa Mungu uko ndani ya Mtu . Ufunuo wa Agano la Kale pia ulikuwa katika mifano (hema, dhabihu, n.k.), lakini katika siku hizi za mwisho amesema kupitia Mwanawe (Ebr. 1:1-2). MUHTASARI Kristo, kwa wakati mmoja, amebeba ndani yake ukamilifu wa maagizo ya Agano la Kale, uhalisi wa vivuli na mifano ya Agano la Kale, na utimilifu wa unabii wa Agano la Kale. Kweli zile kumhusu Yeye zinazochipuka katika Agano la Kale zinachanua kikamilifu katika Agano Jipya; mwanga hafifu wa kweli ya kinabii unageuka kuwa mafuriko ya nuru ya ufunuo wa
76
Made with FlippingBook Digital Publishing Software