Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
Mungu. Vivuli vya Agano la Kale vinapata utimilifu wake katika Agano Jipya kwa njia kadhaa: (1) Sheria za maadili za Agano la Kale zinatimizwa au kukamilishwa katika maisha na mafundisho ya Kristo; (2) Kweli za kiibada na za vivuli zilikuwa tu mifano au vivuli vya uhalisi wa kweli unaopatikana katika Kristo; (3) Unabii wa Kimasihi uliotabiriwa katika Agano la Kale hatimaye ulitimizwa katika historia ya Agano Jipya. Katika kila moja ya mahusiano haya tunaweza kuona kwamba maagano haya yameunganishwa kwa namna isiyoweza kutenganishwa. Agano Jipya si tu kwamba linatimiliza lile la Kale bali pia linalikamilisha. Kama vile kitabu cha Waebrania kinavyosema, “kwa kuwa Mungu alikuwa ametangulia kutuwekea sisi kitu kilicho bora, ili wao [waamini wa Agano la Kale] wasikamilishwe pasipo sisi” (Ebr. 11:40). Kwa maana yale yaliyomo katika Agano la Kale yamefafanuliwa kikamilifu tu katika Agano Jipya.
77
Made with FlippingBook Digital Publishing Software