Kristo: Mada Kuu Ya Biblia
SURA YA 4 | KRISTOKATIKA KILA SEHEMU YA BIBLIA KRISTO PIA NDIYE UFUNGUO wa muunganiko wa muundo wa Biblia. Mtazamo wa Kristo kama kiunganishi cha kimuundo kati ya maagano haya mawili tayari umejadiliwa katika sura iliyotangulia; hapa Kristo atawasilishwa kama mada inayounganisha sehemu mbalimbali za Biblia. KRISTO KAMA MSINGI: MGAWANYO WA MAANDIKO KATIKA SEHEMU NNE Sehemu Mbili za Agano la Kale Tangu nyakati za kale Biblia iligawanywa katika sehemu za msingi. Mojawapo ya migawanyo iliyozoeleka zaidi, na pengine wa kwanza kabisa, ulikuwa ni mgawanyo wa Agano la Kale katika sehemu mbili – Torati na Manabii. Torati, ambayo Musa aliandika, iliwekwa katika fungu la peke yake, na kila kitu kilichokuja baada ya hiyo kiliitwa Manabii. Torati ya Musa Kutokana na ushuhuda wa kundi kubwa la waandamizi wa Musa katika Biblia, ni dhahiri kwamba Musa ndiye aliyeandika Torati na kwamba iliwekwa katika tabaka la peke yake. Kwanza, ikumbukwe kuwa Musa mwenyewe alisema kwamba aliandika Torati kama vile Mungu alivyomfunulia (rej. Kut. 20:1; 35:1; Hes. 1:1; 36:13). Aliwaonya watu, “Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za Bwana, Mungu wenu, niwaamuruzo” (Kum. 4:2). Na “Basi ikawa hapo Musa alipomaliza kuandika maneno ya torati hii katika chuo, hata yakaisha, 25 ndipo Musa akawaamuru Walawi waliokuwa wakilichukua sanduku la agano la Bwana akawaambia, 26 Twaeni chuo hiki cha torati, mkiweke kando ya sanduku la agano la Bwana, Mungu wenu, ili kiwepo kama shahidi juu yako” (Kum. 31:24-26).
78
Made with FlippingBook Digital Publishing Software