Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 1 0 1
K U T A F S I R I B I B L I A
MUUNGANIKO
Kufikia ustadi na umahiri katika Neno la Mungu ni jambo la msingi na hitaji muhimu sana kwa kila mwanamume na mwanamke mtumishi wa Mungu, kwa sababu ni maandiko yenye pumzi ya Mungu pekee yanayoweza kutufanya watenda kazi hodari na watumishi waaminifu wa Kanisa, ili kutuwezesha kuwaandaa wengine kwa ajili ya huduma, na kuhudumia mahitaji halisi ya wale walio ndani na nje ya Kanisa (2 Tim. 3:16-17). Hakuna namna bora tunayoweza kukazia sana umuhimu wa uwezo wako wa kulitumia Neno kwa usahihi ( 2 Tim. 2:15 ), kutafakari juu Neno mchana na usiku ili uweze kufanikiwa katika yote utendayo kwa ajili ya Mungu ( Yos. 1:8 ), na kuwa na uhakika juu ya aina ya matokeo na nguvu unayotamani katika kila hatua ya utumishi wako kwa Bwana (Zab. 1:1-3). Zifuatazo hapa chini ni dhana kuu ambazo tumejifunza katika somo hili la Mbinu ya Hatua Tatu , kwa hivyo tafadhali zipitie kwa bidii na kwa umakini. Kuelewa mbinu hii kunaweza kukuwezesha kupata ujuzi na ustadi wa kuwa mtenda kazi wa maandiko, mwenye kukubaliwa na Mungu na usiye na sababu ya kutahayari unapotulimia Neno lake kwa usahihi na uhalali. ³ Mbinu ya Hatua Tatu ni mbinu fasaha ya kutafsiri Biblia iliyotengenezwa ili kutusaidia kuelewa kweli ya maandiko na kuziba pengo lililopo kati ya ulimwengu wa kale na wa sasa. Mbinu ya Hatua Tatu inafafanuliwa kama “kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza ya andiko ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu.” ³ Ingawa kusoma maneno mahususi, vifungu vya maneno, aya, sura, sehemu, na vitabu vya Biblia ni jambo la kujenga na la lazima, ufahamu wetu wote katika maandiko unapaswa kuendana na ujumbe wa Biblia nzima, yaani, maana na ujumbe wa ufunuo wa mwisho wa Mungu kwetu katika nafsi na kazi ya Yesu Kristo. ³ Mbinu ya Hatua Tatu inaakisi na kuendana na mbinu ya sarufi ya kihistoria ya kutafsiri maandiko, ambayo inahakiki na kuthibitisha maana ya wazi ya maandiko katika Biblia, ufunuo endelevu wa Mungu kwa njia ya Kristo, umoja wa Biblia, na usahihi wa andiko katika kuwasilisha ujumbe kwetu kwa kutumia tanzu na miundo tofauti ya fasihi. ³ Kila hatua inayohusika katika Mbinu ya Hatua Tatu ina lengo na mantiki yake mahususi, kadhalika ina sababu na msingi, na mitazamo muhimu, na inatimizwa kwa fuata mpangilio na orodha maalum ya vipengele. Ili kuweza kutumia mbinu hii lazima tuwe na ufahamu na ujuzi kuhusiana na hatua husika na vipengele vyake.
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Umuhimu wa Msomaji wa Kwanza: Ufunguo wa Mbinu ya Hatua Tatu. Wafasiri na wakalimani wanapojiuliza ni kwa namna gani wasomaji wa kwanza wangeelewa kifungu fulani, hawaulizi swali la kidhahania tu ambalo haliwezekani na fikra zao). Badala yake, hii ni njia rahisi ya kutupeleka kwenye maswali mengine madogo: Je! Maneno haya yangeelewekaje wakati huo? Ni maswala na mada gani zilikuwa za umuhimu mkubwa? Andiko hili la Biblia lingeweza kukabiliana na aina gani ya mfumo wa fikra? Kuuliza maswali kama haya hakumaanishi kwamba tunaweza kupata majibu kamili wakati wote. Wakati mwingine tunaweza kukisia majibu sahihi kwa kuyalinganisha maandiko yenyewe. ~ Donald A. Carson. New Bible Commentary: 21st Century Edition. (electronic ed. of the 4th ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1997. kujibu (kwa kuwa hatuna uwezo wa kuingia katika akili
2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker