Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
1 0 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
2. Kwa nini siku zote ni muhimu kuanza vipindi vyetu vya kujifunza Neno la Mungu kwa kusali kwa Mungu ili kupata hekima, mwongozo, na maelekezo? Tunawezaje kuomba kwa namna ambayo hatutafanya hivyo kwa mazoea na kuondoa mantiki nzima ya maombi, na badala yake yawe maombi halisi ya kupokea hekima ambayo ni Mungu pekee awezaye kutuandalia tunapojifunza Neno lake? 3. Kwa nini haiwezekani kutambua maana ya kifungu cha maandiko bila msaada wa RohoMtakatifu (taz. 1Kor. 2:9-16)? Hata hivyo, kwa nini kuomba maongozi ya Roho Mtakatifu kamwe hakuwezi kuwa mbadala wa kujifunza Neno la Mungu kwa bidii na kwa nidhamu kama fasihi ? Elezea jibu lako. 4. Tulitumia zana gani katika hatua yetu ya kwanza ya Mbinu ya Hatua Tatu katika ufafanuzi wa 1 Wakorintho 9:1-14? Je, zana hizi zinatusaidiaje kuelewa vizuri zaidi muktadha wa awali wa andiko, yaani, kile ambacho Paulo alikusudia kuwaelekeza Wakorintho katika muktadha wao? 5. Je, ni aina gani za maswali ambayo tunapaswa kuuliza tunapotafuta kutambua muktadha wa asili ambamo kifungu kiliandikwa? Je, tunawezaje kujibu maswali hayo? 6. Fafanua maana ya “kanuni ya jumla ya maandiko.” Je, kauli kama hizi za muhtasari kama mithali, misemo, na kanuni nyingine za jumla husaidiaje kutupa ufahamu kamili zaidi wa mapenzi ya Mungu? 7. Toa mifano ya kauli tatu za muhtasari au kanuni za jumla katika Biblia. Unawezaje kujua kwamba kanuni uliyoitengeneza kama matokeo ya muda wako binafsi wa kujifunza Neno ni kanuni ya maandiko? Je, unapaswa kufanya nini ili kuthibitisha kwamba ulichokigundua kwa hakika ni kanuni ya Neno? 8. Kwa nini ni lazima tutafute nia ya Mungu tunapotumia maana za Biblia kwa vitendo katika maisha yetu? Uhuru una nafasi gani katika kuonyesha utii wa mioyo yetu kwa Mungu tunapoitikia mafundisho yake katika maandiko? 9. Kwa nini sikuzote ni muhimu kukumbuka ujumbe mpana zaidi wa maandiko kuhusu Kristo na Ufalme wake tunapotafuta kutumia Neno la Mungu maishani mwetu? Ni makosa ya aina gani yanaweza kutokea ikiwa tutashindwa kumfanya Kristo kuwa kiini cha kila hatua ya usomaji wetu na matumizi ya maandiko? (Someni pamoja Yohana 5:30-47 na jadilini karipio la Yesu mwenyewe kwa Mafarisayo kuhusu aina hii ya mazoea, ya kusoma Biblia na bado wakashindwa kumwona Kristo kama kiini cha ujumbe wa maandiko).
2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker