Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 1 8 /

K U T A F S I R I B I B L I A

2 Tim. 3:16-17, “Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.” Tunawezaje kutumia ufahamu wetu wa kanuni za fasihi kuboresha ujuzi wetu wa Neno la Mungu, na wakati huo huo kutofanya iwe vigumu kwa watu wote kufahamu maana ya maandiko isipokuwa kwa wataalamu wabobevu?

Namna za Kizamani.

Karibu na mwanzo wa karne hii, wasomi wengi wa kiinjili walizingatia zaidi vivuli vya Biblia. Kivuli ni mfano wa awali wa Kristo katika Agano la Kale ambao umefunuliwa katika Agano Jipya. Kwa mfano, Melkizedeki ni kivuli (mfano) cha Kristo, kwa maana Kristo ndiye Kuhani Mkuu wa Kanisa. Mana inaonekana kama kivuli cha Kristo, ambaye ni mkate wa uzima (Yohana 6), nyoka ambaye Musa alimwinua juu ya mti jangwani kwa agizo la Mungu kwa ajili ya uponyaji wa watu ni kivuli (Yohana 3:14-15). Namna hii ya kumtafuta Kristo katika vivuli, wahusika, na picha za Agano la Kale (k.m., Hema la Kukutania, ukuhani wa Walawi, na dhabihu zilizoandikwa katika Agano la Kale), sasa inaonekana na wasomi wengi kama haifai na haina umuhimu. Kwa sababu ya kutia chumvi kwingi na tafsiri potofu za wengi waliotumia njia hii, sasa ule mkazo wa kuhusianisha picha na hadithi za Agano la Kale na Yesu Kristo si jambo linalokubalika kama ilivyokuwa zamani. Unafikiri kwamba hii bado inaweza kuwa mbinu sahihi, au aina hii ya hemenetiki ya Biblia imepitwa na wakati? Tunapaswa kufanya nini kuhusiana na hadithi, picha, sitiari na taashira zote hizi za maandiko zinazohusiana na Yesu Kristo? Kwa namna ambayo wahubiri wengi siku za leo wanatilia mkazo zaidi katika mafundisho, mawazo, dhana, na maarifa, wengi wao wamepoteza ile hali ya kuvutiwa na nguvu ya hadithi. Ingawa taaluma mpya ya theolojia (iitwayo “theolojia simulizi”) inayozingatia hadithi inapata makao mapya katika elimu ya Biblia, wahubiri na walimu wengi bado wanapendelea maelezo rahisi, mafupi na ya moja kwa moja ambayo yanaeleza wazi ni kisa gani, tukio gani au taashira gani inayoongelewa. Kwa kuwa wanatumia muda mchache kwenye mimbari zao au darasani, wahubiri na walimu wengi wanalazimika kutumia muundo wa takriban dakika 30 katika uwasilishaji, jambo ambalo linawapa muda mchache sana wa kusoma kifungu na kisha, kwa maelezo mafupi ya moja kwa moja, kufanya muhtasari wa kile wanachoamini kuwa maana ya kifungu hicho cha maandiko. Hata hivyo, namna hii ya ufundishaji inaweza kuwa na matatizo yake, kwa kuwa Ni kipi kililokuja kwanza: Hadithi au fundisho?

2

3

3

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker