Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 1 9

K U T A F S I R I B I B L I A

wengi wanaona kwamba uwasilishaji katika mfumo wa simulizi ndio muundo wa msingi zaidi wa ufunuo katika Biblia. Kwa maneno mengine, Mungu anapotaka kuwasiliana nasi kuhusu asili ya kweli fulani au tukio fulani, kwa kawaida husimulia hadithi, ama zinazotokana na matukio halisi ya kihistoria au zilizobuniwa kwa faida ya kielelezo na uchambuzi. Ni aina gani ya kujifunza Biblia ambayo ni ya msingi zaidi kwako: simulizi au uwasilishaji wa moja kwa moja wa fundisho? Je, ni muhimu kutumia muda mwingi kujifunza njia za hadithi, na kutafuta ujumbe wa Mungu katika hadithi, au kwenda tu katika sehemu za maandiko ambapo mawazo ya Mungu yamefafanuliwa moja kwa moja na kwa uwazi (k.m. Nyaraka)? Ni kipi kinapaswa kuja kwanza, hadithi au fundisho?

Fasihi ya Kibiblia: Kutafsiri tanzu za kibiblia Sehemu ya 1: Kanuni za Jumla za Ufasiri

YALIYOMO

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

3

Neno “tanzu” linarejeleamuundomaalumwa fasihi ambao umetumika kuwasilisha Kweli na lazima utafsiriwe kulingana na kanuni za muundo huo. Utafiti wa tanzu ni muhimu kwa ufasiri mzuri wa Biblia kwa sababu Biblia yenyewe kama kitabu cha fasihi imejaa aina mbalimbali za fasihi, ambazo zote zinafanya kazi kulingana na kanuni maalum. Mungu amewasiliana nasi kwa kutumia miundo ya fasihi na tanzu za lugha za kibinadamu ili kuwasilisha Neno lake. Mambo hayo yanahusisha matumizi ya masimulizi (ya kihistoria na ya kutunga), Sheria (maandiko ya kisheria), nyaraka (barua), unabii, fasihi ya hekima (methali, monolojia, vitendawili, hekaya, mafumbo, istiari, n.k.), na ushairi. Aina za uwasilishaji wa fasihi hutofautiana kwa sababu ya msukumo wa kutimiza hitaji fulani katika muktadha fulani, kuongeza uelewa wetu wa msingi wa maisha ya mwanadamu, kutuwezesha kupata picha ya uhalisia katika sura yake kamili, kuonyesha ufundi wa waandishi wa Biblia kama walivyoongozwa na Roho, na kufunua utajiri wa siri ya Mungu na kazi yake ulimwenguni. Kujifunza tanzu na matumizi yake kunaweza kutuimarisha na kututia nguvu tunapotafuta kuelewa maana ya Neno la Mungu. Lengo letu la sehemu hii, Kanuni za Jumla za Ufasiri , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno “tanzu” linarejelea muundo maalum wa fasihi ambao umetumika kuwasilisha Kweli na lazima utafsiriwe kulingana na kanuni za muundo huo. • Kazi ya kutafsiri Biblia kwa kuzingatia matumizi ya tanzu lazima ianze kwa ufahamumakini wa dhana za msingi za elimu ya tanzu, ambayo inathibitisha

Muhtasari wa Sehemu ya 1

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker