Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 2 1

K U T A F S I R I B I B L I A

I. Muhtasari wa dhana ya “Tanzu”.

Muhtasari wa Sehemu ya 1 ya Video.

A. Ufafanuzi

1. “Aina ya utunzi wa kisanii, kama ilivyo katika muziki au fasihi, inayotambulika kwa mtindo, muundo, au maudhui mahususi” ( American Heritage Dictionary of the English Language )

2. Tanzu za Biblia = “Aina tofauti tofuati za uandishi zinazopatikana ndani ya vitabu vya Biblia, zote zikitokana na chanzo kimoja na uvuvio mmoja katika Mungu, huku zikifunua kweli yake na mapenzi yake kwa kutumia njia tofauti za uwasilishaji, katika namna ya kukamilishana.”

3

3. “Tanzu” ni istilahi ya kifasihi yenye maana ya aina au namna fulani ya uandishi. . . “Mtazamo wa kifasihi kuhusu Biblia unajengwa juu ya ufahamu kwamba fasihi yenyewe ni tanzu” (Leland Ryken).

4. “Kundi au kategoria ya jitihada za kisanii zenye muundo, maudhui na mbinu mahususi” (Webster’s Unabridged).

5. Utanzu wa kibiblia ni muundo fulani wa fasihi ambao unawasilisha ukweli na lazima utafsiriwe kulingana na kanuni za muundo huo .

B. Mawazo ya msingi

1. Biblia ni fasihi: kila kitabu cha Biblia kimeundwa kwa uangalifu na waandishi wake ambao ni Mungu na wanadamu.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker