Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 2 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

a. Waandishi walichaguwa mambo ya kuandika kutoka kwenye hazina ya uzoefu ambao wangeweza kuuandika. Yoh 21:24 25 – Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya: nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. 25 Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa. b. Waandishi hufanya kazi kama wahariri. 2 Nya. 24:27, “...maelezo katika kitabu cha wafalme”; mwandishi wa kitabu cha Mambo ya Nyakati wa Pili anarejelea maandishi ya Nathani na Ahiya (9:29), Shemaya (12:15), Yehu (20:34), na vitabu viwili tofauti vya Ido (9:29 na 13:22) kama sehemu ya vyanzo ambavyo alivitumia kutengeneza kitabu chake.

c. Mambo yaliwekwa pamoja ili kuwasilisha ukweli kadri iwezekanavyo kwa njia ya uhakika na yenye matokeo, Luka 1:1-4.

3

2. Biblia imetumia lugha katika namna ya kifasihi (sio tu kama ripoti ya maelezo au nathari).

a. Sitiari na tashbihi – Ufalme wa Mungu ni kama mfanyabiashara anayetafuta lulu, kama punje ya haradali, kama wavu, nk.

b. Picha na taashira – picha ni neno linalotaja kitu halisi, na taashira ni kitu ambacho kinasimama mahala pa kitu kingine kama kidokezo cha maana yake halisi (mafuta, moto, maji, kaya, matunda, kichwa).

c. Vivuli na vivuli vikuu – vivuli vikuu ni mambo yanayofahamika na wanadamu ulimwenguni kote (jua, familia, magugu, simba), yaani, ni alama za ulimwengu wote. Vivuli ni matukio, watu, na mahali katika historia ya wokovu ambavyo vinasimama kama mfano wa vitu vitakavyotokea wakati ujao (k.m, Yusufu ni kivuli cha Yesu: anauzwa kwa vipande 30 vya fedha, anaokoa familia yake,

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker