Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 2 3

K U T A F S I R I B I B L I A

anathibitishwa na Mungu na kuinuliwa katika nafasi ya mamlaka mkono wa kuume wa Farao).

3. Tanzu zinaashiria kwamba kweli ya Mungu inaweza kuwasilishwa katika miundo mbalimbali ya uandishi wa kifasihi, ambayo yote, licha ya tofauti zake, imevuviwa na Mungu na inawasilisha ujumbe wake katika Kristo.

II. Miundo ya tanzu za kibiblia – Ni miundo ipi muhimu zaidi ya tanzu za Biblia tunayoweza kujifunza?

Uhakiki wa kifasihi unalenga zaidi uchambuzi wa tanzu katika kujifunza Biblia. Uhakiki wa kifasihi pia unatambua uwepo wa miundo au tanzu mbalimbali za fasihi ambazo zawezakuwa zilitumika katika uandishi wa Biblia. Kwa namna fulani, kuna vitabu vizima ambavyo ni vya utanzu wa aina moja, kama vile simulizi ya kihistoria (1 Samweli), mashairi (Zaburi), hekima (Ayubu), hotuba ya kinabii (Amosi), Injili (Mathayo), barua (Warumi), au apokalipsi (Ufunuo). Hata hivyo ndani ya kazi hizi kubwa inapatikana miundo midogo ya kifasihi: hekaya za uumbaji; nasaba; simulizi zinazohusu hadithi za watu binafsi, kama vile Ibrahimu au Yusufu; kanuni za kisheria; maagano; zaburi; mithali; hotuba za kinabii; hadithi za miujiza; mafumbo; maombi; nyimbo; mawaidha; na maonyo. Orodha hii si ya kina, lakini inaashiria kwamba Biblia, badala ya kuwa kazi ya kifasihi yenye utanzu wa aina moja, ina aina tofauti za tanzu na vipera vya semi. ~ R. Holladay. “Biblical Criticism.” Harper’s Bible Dictionary . P. J. Achtemeier, ed. (1st ed.) Harper & Row: San Francisco, 1985, p. 131.

3

A. Simulizi – hadithi za matukio na wahusika katika Biblia, ama za kihistoria au za kufikirika (kutunga).

1. Aina za masimulizi

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker