Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 2 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

a. Simulizi za kihistoria – k.m., hadithi za Agano la Kale, Matendo, Injili, simulizi za ufufuo.

b. Simulizi ya kufikirika – k.m., mifano, kama wa mwana mpotevu, n.k.

2. Wahusika – Nani anaigiza au anaigizwa?

3. Mazingira – Uigizaji unafanyika wapi?

4. Dhamira – Dhamira ya jumla ya hadithi hii inahusu nini

5. Ploti – Mtiririko wa hadithi ukoje katika simulizi husika?

3

6. Kanuni – Ni kweli gani zinazoweza kupatikana katika hadithi, ambazo zina mvuto na umuhimu kwa watu wote?

Simulizi (kusimulia hadithi) ni njia kuu ambayo Mungu ameichagua ili kuwasiliana na sisi, na hazikusudiwi tu kuwasilisha habari dhahania, bali kutuhusisha katika unyeti na utajiri wa uzoefu wa maisha ya mwanadamu, na hivyo kutupa mwangaza katika mambo ya maisha yetu wenyewe.

B. Sheria (maandiko ya kisheria) – amri na kanuni katika maandiko zinazoelezea matakwa, makatazo, na masharti ya mapenzi ya Mungu katika muktadha fulani.

1. Aina za sheria

a. Sheria za lazima (“Fanya hivi”)

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker