Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
1 3 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Fasihi ya Kibiblia: Kutafsiri Tanzu za Biblia Sehemu ya 2: Kufasiri simulizi na tanzu za unabii katika maandiko
Mchungaji Dkt. Don L. Davis
Neno “Hemenetiki maalum” linazungumzia sheria na taratibu maalum zinazotuwezesha kufasiri aina za fasihi ya Biblia. Hemenetiki kama hiyo ni muhimu, hasa tunapoanza kutumia kanuni hizi katika ufasiri wetu wa aina mbalimbali za fasihi ya Biblia. Simulizi ni aina mahususi ya ujuzi, na ndio msingi wa theolojia ya hadithi, ambayo hoja yake ya msingi ni kwamba Mungu alitoa maelezo ya kazi yake kupitia simulizi za hadithi za Biblia. Wanatheolojia wa hadithi wanatambua umuhimu wa hadithi, namna ambavyo (miongoni mwa mambo mengine) hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti, zinakubalika kama msingi wa maongozi katika Jamii ya Kikristo, na hutoa theolojia, liturijia, na sakramenti. Unabii ni utanzu mwingine wa ufasiri wa Biblia, ambao unawasilisha ukweli kuhusu Mungu na ulimwengu, na unajidhihirisha kupitia mtu au kwa njia ya fasihi. Fasihi ya kiapokaliptiki ni kijitanzu (tawi dogo) cha unabii, kipengele kinachoonekana katika aina mbili kuu za apokalipsi za Kiyahudi, katika kitabu cha Agano la Kale cha Danieli, na kitabu cha apokaliptiki kilicho dhahiri zaidi katika maandiko, yaani kitabu cha Ufunuo. Tutafasiri tanzu za unabii na za kiapokaliptiki za maandiko vizuri ikiwa tutazingatia umuhimu wa kuweka mkazo zaidi kwa Yesu Kristo, kuelekeza jumbe za kinabii katika wito wa Ufalme wa Mungu, na kusisitiza juu ya kutimia kwa makusudi makuu ya Mungu hata katika nyakati za uovu, mateso na ukosefu wa haki. Lengo letu katika sehemu hii, Kufasiri simulizi na tanzu za unabii katika maandiko , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Neno “Hemenetiki maalum” linazungumzia sheria na taratibu maalum zinazotuwezesha kufasiri aina za fasihi ya Biblia. • Simulizi ndio aina ya tanzu iliyoenea zaidi katika maandiko, na inajumuisha hadithi na simulizi za hadithi ambazo ni za kihistoria na zilizotungwa (za kufikirika). • Wanatheolojia wa hadithi hujikita katika simulizi za hadithi katika maandiko, na kuanza kazi yao ya kufasiri kwa dhana ya jumla ya theolojia ya hadithi, ambayo ni pamoja na wazo kwamba njia ya kuu ambayo Mungu ameitumia kuelezea asili yake na kazi yake ni kupitia simulizi za hadithi katika maandiko. Dhana nyingine ni pamoja na wazo kwamba theolojia yote ni tafakuri ya hadithi za Biblia, kwamba hadithi za Biblia
Muhtasari wa Sehemu ya 2
3
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker