Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 3 9

K U T A F S I R I B I B L I A

zinazorejelea simulizi za kihistoria ni za kuaminika na sahihi, kwamba hadithi zimeandikwa kwa ustadi wa kisanii, kwamba tunakutana na Mungu kupitia hadithi za Biblia, na kwamba mara nyingi Mungu hutoa ufafanuzi wake mwenyewe kuhusu maana ya simulizi za hadithi za Biblia. • Theolojia ya hadithi imejengwa juu ya msingi wa dhana muhimu kuhusu hadithi, Biblia, na Kanisa. Hizi ni pamoja na dhana kwamba hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti, ni muhimu zaidi kuliko maelezo ya kawaida, zinakubalika kama msingi wa maongozi katika jamii ya Wakristo. Tamaduni za Kikristo hukua na kujifafanua zenyewe kwa njia ya hadithi, ambazo hutangulia na kuzaa jumuiya, maonyo na uwajibikaji, na huzalisha theolojia, liturjia na sakramenti. Hadithi ni historia. • Kama fasihi nyingine, vipengele vya jumla vya simulizi katika maandiko ni pamoja na mazingira, wahusika, mtazamo wa mwandishi, mtiririko (ploti), na dhamira ya hadithi. • Unabii ni tanzu nyingine kuu ya maandiko, aina ya fasihi ambayo inawasilisha ukweli kuhusu Mungu na ulimwengu, unatokana na Roho na ni njia maalum ya ufunuo kutoka kwa Mungu ambayo inajidhihirisha kupitia mtu au kwa njia ya fasihi. • Apokaliptiki ni kijitanzu (tawi) cha unabii, na inajumuisha aina mbili kuu za apokalipsi za Kiyahudi, kitabu cha Agano la Kale cha Danieli, na kitabu cha apoliptiki kilicho dhahiri zaidi katika maandiko, yaani kitabu cha Ufunuo. • Ili kutafsiri kwa usahihi tanzu za unabii na za kiapokaliptiki za maandiko, ni lazima kwanza tuzingatie umuhimu wa kuweka mkazo zaidi kwa Yesu Kristo, kuelekeza jumbe za kinabii katika wito wa Ufalme wa Mungu, na kusisitiza juu ya kutimia kwa makusudi makuu ya Mungu hata katika nyakati za uovu, mateso na ukosefu wa haki.

3

Utofauti katika Maandiko

Katikati ya umoja wa maandiko, hatupaswi kupoteza mtazamo wa utofauti wake. . . Hili linahusisha aina kadhaa. Vitabu vya Biblia vimeandikwa na waandishi tofauti, katika nyakati na mahali tofauti, kwa hadhira tofauti katika mazingira tofauti, kwa kutumia aina tofauti za fasihi. Kwa hivyo kila kitabu kinaonyesha madhumuni na dhamira (mada) za kipekee. Nyakati fulani, unakutana sehemu tofauti za maandiko zizonalingana kwa ukaribu sana kiasi kwamba tunaweza kuzihusianisha kifasihi na kudhani kwamba tofauti zake ni za makusudi: wakati mwingine kwa

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker