Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 1 4 1
K U T A F S I R I B I B L I A
3. Utanzu wa kibiblia ni muundo maalum wa fasihi ambao unawasilisha ukweli na lazima ufasiriwe kulingana na kanuni za muundo huo.
4. Hemenetiki maalum ni tawi la ufasiri wa kibiblia lenye lengo la kuelewa na kutumia kanuni mahususi za ufasiri zinazohusiana na kila muundo kwa kuzingatia namna ya uwasilishaji wa muundo husika.
B. Simulizi (hadithi) katika fasihi.
1. Simulizi katika mfumo wake wa kifasihi hutambulika kwa “uwepo wa hadithi na msimuliaji wa hadithi” (Robert Scholes na Robert Kellogg, Nature of Narrative , London: Oxford University Press, 1966, p. 4).
2. “Hadithi . . . [ni] simulizi ya wahusika na matukio katika mtiririko (ploti) inayoendelea katika wakati na nafasi kupitia katika mzozo kuelekea utatuzi” (Gabriel Fackre, “Narrative Theology”).
3
3. Simulizi ni hadithi, ziwe za kihistoria (hadithi kuhusu mambo ambayo yalitokea kweli) au za kufikirika (hadithi za kubuni ambazo Mungu au watu katika maandiko wamesimulia, kwa kawaida ili kueleza ukweli wa kiroho au kutoa changamoto yenye fundisho la kiroho). Mafumbo (au mifano katika Biblia) ni mfano mzuri wa dhana hii.
C. Dhana za jumla za theolojia ya hadithi.
1. Mungu ametupa ufunuo kuhusu tabia yake na matendo yake hasa kupitia simulizi za hadithi za Biblia.
a. Sehemu kubwa ya maandiko katika Neno lake iko katika mfumo wa hadithi.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker