Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
1 4 2 /
K U T A F S I R I B I B L I A
b. Ufahamu wa njia ambazo hadithi hutenda kazi unaweza kusaidia na kuongeza ujuzi wetu wa Biblia, na kwa njia hiyo tunaweza kumfahamu Mungu wa Biblia.
2. Theolojia yote ni tafakuri ya hadithi za Biblia, na ni elimu ya “ngazi ya tatu”.
a. Ngazi ya kwanza : Mungu na utendaji wake katika historia.
b. Ngazi ya pili : Mungu alisimamia kurekodiwa kwa matendo yake katika historia katika mfumo wa hadithi ndani ya Neno la Mungu.
c. Ngazi ya tatu : tafakuri yetu juu ya Neno ili kufahamu maana ya tabia na matendo ya Mungu.
3
d. Theolojia inaangazia maana ya matendo ya Mungu katika historia yaliyorekodiwa katika hadithi za Biblia.
3. Ingawa hadithi ni vipande vya fasihi vilivyotungwa, hadithi za Biblia ni za kuaminika na sahihi zinaporejelea simulizi za kihistoria.
a. Aina za hadithi (1) Simulizi za kihistoria – zinashuhudia kwa usahihi matukio halisi yaliyotukia, k.m., kuzaliwa kwa Yesu, Luka 2:1-7. (2) Simulizi za kufikirika – ni hadithi zilizobuniwa na mwandishi kwa ajili ya kielelezo na mafundisho, k.m., hadithi ya Nathani kwa Daudi, 2 Sam. 12:1-7.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker