Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 1 4 3
K U T A F S I R I B I B L I A
b. Usahihi wa taarifa za kihistoria katika simulizi za kihistoria za Biblia: utangulizi wa kitabu cha Luka na Matendo ya Mitume, Luka 1:1-4.
4. Waandishi wa maandiko waliandika hadithi zao kwa ustadi wa kisanii kama wasimulizi mahiri.
5. Kusudi la kujihusisha na kujifunza hadithi takatifu ni kukutana na Mungu kupitia maandiko na kuitikia kwa imani na utii tendo hilo, Yakobo 1:22-25.
a. Simulizi zinaonyesha matendo ya Mungu katika historia na kutuelekeza namna anavyotaka kuhusiana nasi leo.
3
b. Ulinganishi wa imani : “Kama vile Mungu alivyokuwa pamoja nao huko wakati huo, ndivyo alivyo na atakavyokuwa nasi daima hapa, sasa.”
c. Hadithi ni kwa ajili ya kukutana: kuhusianisha hadithi [ya Mungu] na hadithi yetu ni ufunguo wa ufahamu juu ya utendaji wa simulizi za Biblia.
6. Mungu mara nyingi hutoa ufafanuzi wake mwenyewe juu ya maana ya hadithi zake ndani ya Hadithi yenyewe.
D. Kauli muhimu kuhusu theolojia ya hadithi William J. Bausch anaorodhesha kauli kumi kuhusiana na theolojia ya hadithi ambazo zinatusaidia kuelewa maana na umuhimu wa elimu ya hadithi na uelewa wa Biblia na theolojia. (William J. Bausch, Storytelling and Faith . Mystic, Connecticut: 23rd Publications, 1984.)
1. Hadithi hutuleta katika uwepo wa kisakramenti.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker