Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 1 5 5

K U T A F S I R I B I B L I A

C. Apokaliptiki ya AJ: kitabu cha Ufunuo.

Ujumbe unaoongoza kwa Yesu Kristo.

Biblia haikutoka katika sehemu moja kama kitabu cha mafundisho au mwongozo wa maadili. Badala yake, ikijumuisha aina mbalimbali za fasihi, ni rekodi ya historia ya ufunuo maalum, historia ambayo utengenezaji wake wenyewe (uandishi . . . ) ni sehemu yake. Historia hii ndefu inaanza mapema enzi za bustani ya Edeni na, baada ya anguko, inaendelea kama shughuli ya Mungu ya ukombozi inayoendelea, ikiambatana na neno lake mwenyewe la uthibitisho na ufasiri, hasa katika shughuli zake za kiagano na Israeli, hadi kilele chake katika maisha na kazi ya Kristo. Kwa sababu hiyo, ufunuo wa kibiblia, kimsingi ni wa ukombozi, au wa kimaagano- kihistoria, na shughuli ya theolojia ya Biblia ni kuchunguza na kufafanua tabia hii ya kihistoria endelevu na ya tofauti ya ufunuo maalum. ~ R. B. Gaffin “New Testament Theology.” New Dictionary of Theology . Sinclair B. Ferguson, David Wright, eds. (electronic ed.). Downers Grove, IL: InterVarsity Press, 1988, p.463.

1. Apokalipsi pekee ya kweli katika Agano Jipya (rej., Shepherd of Hermas , iliyoandikwa na nabii Mkristo).

2. Kimetokana na mapokeo ya kihistoria kuhusu eskatolojia ya apokalipsi za Kiyahudi.

3. Kinashughulika na nia ya Mungu ya kutahadharisha Kanisa lake kuhusu matukio yatakayotokea, Ufu. 1:1-3.

4. Kinatoa ufunuo wa kina wa maisha na kazi ya Yesu Kristo, Ufu. 1:7 18.

3

5. Kinaelezea masuala ya hukumu mwishoni mwa historia ya mwanadamu, Ufu. 20:11-15.

6. Kinatumia lugha ya fumbo na ya kufikirika ya sitiari, taashira, na fantasia, Ufu. 12:14-16.

7. Inawekea mkazo umuhimu wa nambari na seti za nambari katika kuunda na kuwasilisha maudhui ya ujumbe; kwa mfano, Ufu. 13:18; 21:12-14; 4:2-8.

V. Kanuni tatu za ufasiri wa tanzu za kinabii na kiapokaliptiki:

A. Kanuni ya kwanza: Weka mkazo kwa Yesu Kristo .

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker