Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
1 7 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
wa Biblia, na pia kutoa mapendekezo kwa kila moja ya zana hizo ambayo yanaweza kuboresha kazi yetu ya ufafanuzi wa maandiko. • Kubainisha umuhimu ya visaidizi vya rejea mtambuka ( cross-reference ) katika ufafanuzi wa Biblia (k.m., Biblia za mada, Biblia zenye rejea mtambuka, na miongozo ya mada na konkodansi), kufafanua faida zake katika kujifunza, na kuelezea baadhi ya tahadhari muhimu tunazopaswa kufahamu tunapotumia zana kama hizo. • Kuonyesha sababu za kutumia kamusi za Biblia, ensaiklopidia, atlasi, na vitabu vya mwongozo wa Biblia vinavyoshughulika na desturi na historia, kubainisha manufaa ya zana hizo, na pia tahadhari kuhusiana na matumizi mabaya au kuzitegemea kupita kiasi katika jitihada zetu za ufasiri, na athari zake. • Kunukuu ufafanuzi wa miongozo ya Biblia ( Bible handbooks ), Biblia za kujifunzia ( Study Bibles) na miongozo ya taswira za Biblia ( guides to biblical imagery ), manufaa na taadhari zinazohusiana na matumizi ya zana hizo; kuelezea kwa mifano manufaa na tahadhari hizo kwetu tunapozitumia katika kujifunza Biblia. • Kueleza kwa muhtasari aina kuu za vitabu vya ufafanuzi ( commentaries ) vilivyopo kama visaidizi vya ufasiri wetu (k.m, vitabu vya ibada, mafundisho, eksejesia , na homiletiki ), na kueleza kwa umakini manufaa na tahadhari muhimu zinazohusiana na matumizi ya zana hizo. • Kufanya muhtasari wa mwongozo wa “matumizi bora” ya zana zisizo za kibiblia katika kazi yetu ya kutafsiri Biblia, ukijumuisha jitihada zetu za kujaribu kuziba pengo kati ya ulimwengu wa enzi za maandiko na ulimwengu wetu wa sasa. • Kuelezea mipaka ya zana, yaani, namna ambavyo katika uchambuzi wa mwisho, madai yote yatokanayo na zana zilizotumika yanapaswa kuhakikiwa kwa kina kwa kuyalinganisha na madai ya maandiko yenyewe, na kuhakikisha hakikukubaliki chochote ambacho kinaonekana kupingana na fundisho lililo wazi katika maandiko kuhusiana na Yesu Kristo na kazi yake ya ukombozi.
4
Roho ya uungwana zaidi!
Ibada
Matendo 17:10-12 – Mara hao ndugu wakawapeleka Paulo na Sila usiku hata Beroya. Nao walipofika huko wakaingia katika sinagogi la Wayahudi. 11 Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa walilipokea lile neno kwa uelekevu wa moyo, wakayachunguza maandiko kila siku, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
page 329 2
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker