Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

1 9 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Tafadhali chukua muda wa kutosha kujibu maswali haya na mengine ambayo yameibuliwa na video. Kwa sababu ya kazi yenye bidii ya wasomi wengi wa Biblia, sasa tuna uwezo wa kutumia safu nyingi ajabu za zana za kitaalamu zilizoundwa ili kutoa maarifa katika ulimwengu wa maandiko ya Biblia. Dhamira yetu muhimu kuhusiana na zana hizo za kitaalamu ni kuziba pengo kati ya ulimwengu wetu na ulimwengu wa kale wa nyakati za Biblia, na hivyo kuwa na uwezo bora zaidi wa kutafsiri Neno kwa usahihi katika jitihada zetu za kugundua maana ya maandiko katika muktadha wake wa asili. Unapopotia maswali yafuatayo, hakikisha kuwa unaelewa jukumu na matumizi ya zana za msingi na namna zinavyoweza kuboresha juhudi zetu za kujifunza maandiko. 1. Hali ya sasa ya upatikanaji wa zana za kitaalamu za Biblia kwa umma kwa ujumla ikoje, na ni aina gani ya fursa ambazo zana hizo hufungua kwa wale wanaotafuta kuziba pengo kati ya ujuzi wetu wa ulimwengu huu na ulimwengu wa kale? 2. Eleza maana ya kauli hii: “zana za ufasiri wa Biblia zimeundwa ili kutusaidia kuziba mapengo mbalimbali kati ya ulimwengu wa Biblia na ulimwengu wetu wa sasa.” Kwa nini kuondoa umbali kati ya dunia hizi mbili ni jambo la msingi sana katika kutafsiri Neno la Mungu kwa usahihi na kuelewa maana yake kwetu leo? 3. Kwa nini ni muhimu sana kutathmini zana kulingana na namna ambavyo hasa kinatusaidia kutambua njia ambayo tunaweza kuondokana na pengo fulani katika lugha, utamaduni, au ujuzi kati ya utamaduni wetu na ule wa waandishi wa Biblia na hadhira zao? 4. Orodhesha zana zilizoelezewa kama “zana za msingi za ufasiri wa Biblia” katika sehemu hii. Kati ya zana hizi zote za msingi, ni ipi unaamini kuwa ni muhimu na ya msingi zaidi katika jitihada zozote za ufasiri wa Biblia? Elezea. 5. Biblia iliandikwa katika lugha gani za kale, na kwa nini tunahitaji tafsiri ya lugha hizo? Je, ni baadhi ya sababu zipi zinazofanya iwe vigumu kuunda tafsiri ambayo itatosha kwa waumini wote? Elezea. 6. Tunaweza kuwa na imani kadiri gani katika tafsiri nyingi za kisasa za maandiko? Tunajuaje kwamba hizo ni tafsiri zenye kutegemeka za lugha za awali? 7. Konkodansi, leksimu, na kamusi ya ufafanuzi ni nini, na zinafanyaje kazi katika suala la kuimarisha uelewa wetu wa maandiko ya Biblia? Je, zinapaswa kutumiwaje, na ni tahadhari gani tunapaswa kufahamu tunapozitumia?

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

page 330  3

4

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker