Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 2 1

K U T A F S I R I B I B L I A

Lengo letu katika sehemu hii, Kujiandaa kwa shughuli thabiti ya kutafsiri Biblia, ni kukuwezesha kufahamu kwamba: • Hemenetiki ni taaluma na tawi la maarifa linahusika na ufasiri, hasa ufasiri wa maandiko. Hemenetiki ya Biblia inajikita hasa katika mbinu na sayansi ya kufasiri Biblia. • Kwa namna yoyote ile Biblia lazima ifasiriwe kama kitabu cha kimungu (cha kiroho) na cha kibinadamu, huku tukizingatia kwamba namna zote mbili za kuitazama Biblia (kiroho na kibinadamu) ni za muhimu ili kufahamu na kuelewa kikamilifu asili ya maandiko. • Tangu mwanzo, imani ya Kikristo ya kweli imezingatia dhana fulani za msingi kuhusu asili ya maandiko, ikijumuisha asili yake ya kimungu, ulazima wa andiko kufasiri andiko, dhana ya ufunuo endelevu ambao unafikia kilele katika ufunuo wa Mungu katika nafsi ya Kristo, na ulazima wa utendaji wa Roho Mtakatifu ili kuelewa Neno la Mungu. • Mbinu ya Hatua Tatu ya ufasiri wa Biblia, inayolenga kuchukulia kwa uzito tofauti ya kihistoria na kiisimu (kisarufi) kati ya ulimwengu wa nyakati za Biblia na ulimwengu wetu wa sasa, inahusisha jitihada za kuelewa ujumbe kwa kuzingatia muktadha wake wa asili, kugundua kanuni za Biblia kutoka katika andiko husika, na hatimaye kuhusianisha maana ya andiko na maisha yetu. • Ili kulitafsiri kwa usahihi Neno la Mungu, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili zetu, na nia zetu kulisoma kwa unyenyekevu na kwa uthabiti, kulichanganua kwa uangalifu, na kulitii kwa moyo wote, yote haya kwa ajili ya utukufu wa Mungu. • Tunaandaa mioyo yetu kwa njia ya kunyenyekea na maombi, bidii na kudhamiria, na kujishughulisha kwa bidii katika Neno la Mungu kama mtendakazi. Tunaandaa akili zetu kwa kuchukua majukumu ya mpelelezi, mtafiti, na mwanasayansi – kuchunguza Neno kwa bidii, kufuatilia kwa ukaribu mawazo mbali mbali, na kupima kila ushahidi kwa umakini kabla ya kutoa hukumu. Tunaandaa nia zetu kwa kulitii Neno, si kulisikia tu; na kwa kukumbatia ukweli kwamba hekima inatokana na kuitikia Neno la Mungu, si kulitafakari tu.

1

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker