Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 2 5 5

K U T A F S I R I B I B L I A

K I A M B A T I S H O C H A 2 3 Tamathali za Semi Bob Smith. Basics of Bible Interpretation . Waco: Word Publishers, 1978. uk. 113-120.

Moja kati ya mambo yanayoelimisha zaidi katika lugha ni somo la utumiaji wa tamathali za semi. Profesa Milton Terry anatupeleka katika somo hili Kwa ufahamu wa kina: Utendaji wa asili wa akili ya Mwanadamu unahimiza watu kutazama matukio ya nyuma na kufanya ulinganifu. Hisia za kuridhia zinaamshwa na mawazo yanakuzwa kwa kutumia sitiari na tashbihi. Hata tungetakiwa kutumia lugha inayojitosheleza katikamaneno ili kuelezea dhana zote zinazowekana, badoufahamuwamwanadamu ungetuhitaji sisi kufananisha na kutofautisha dhana hizo na hatua hiyo ingefanya kuwe na ulazima wa matumizi mbalimbali ya tamathali za semi. Maarifa yetu mengi yanapatikana kupitia milango yetu ya fahamu, hivyo mawazo yetu na lugha yetu ya kiroho bado lazima viwe na msingi katika hali ya kimwili. Kama asemavyo Max Muller , “Si vibaya kusema kwamba kamusi yote ya dini ya Kale imejaa sitiari. Kwetu sisi, sitiari zote hizi zimesahauliwa. Tunaongea kuhusu roho bila kufikiria kuhusu pumzi , tunaongea kuhusu mbingu pasipo kufikiria kuhusu anga , tunaongea kuhusu msamaha pasipo kufikiria kuhusu kuachiliwa , tunaongea kuhusu ufunuo pasipo kufikiria kuhusu pazia. Lakini katika lugha ya Kale kila neno katika haya, lilikuwa likitumika, kila neno ambalo lilikuwa halimaanishi kifaa kinachoweza kugusika, bado lipo katika hatua ya ukuaji, nusu kimwili na nusu kiroho, na kuinuka na kuanguka kwa sifa yake kutokana na uwezo wa mzungumzaji wake na wale wanaosikia” 1 Basi, kuna utajiri mkubwa kama nini katika dhana zinazowasilishwa kwa lugha ya kitamathali! Hivyo basi, tukihama na kuzungumza kimahususi kabisa, hebu tuchunguze baadhi ya tamathali za semi. Nitaziorodhesha baadhi ya hizo pamoja na maelezo yake katika kurasa zinazofuata.

1 Profesa Milton S. Terry. Hamenetiki ya Biblia . Grand Rapids: Zondervan Publishing House, n.d. uk. 244.

Tamathali za Semi

TASHBIHI ( Similis = kama)

Ulinganisho rasmi kwa kutumia maneno “kama ilivyo. . .ndivyo ilivyo ” au neno “kama” kuelezea ufanano “ hata hivyo , waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe . . .” (Efe. 5.28).

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker