Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
2 5 6 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Tamathali za Semi (muendelezo)
SITIARI ( Meta + phero = kubeba maana ya)
Ni ulinganisho katika maana, Neno linalotumika katika kitu fulani ambacho sio chenyewe hasa kupendekeza ufanano, mfano “B enjamini ni mbwa-mwitu mwenye kurarua-rarua . . . ” Mwa. 49.27). Mzungumzaji au mwandishi anasema kinyume cha kile ambacho anakusudia kuwasilisha. “. . . hapana shaka ninyi ni ndinyi watu sahihi, nanyi mtakapokufa, ndipo na hekima itakoma ” (Ayubu 12.1-2). Neno moja linatumika sehemu ya neno jingine ili kuonyesha uhusiano fulani uliopo kati ya vitu “ kuua pasaka . . . ” (Kut. 12.21) pale ambapo inamaanisha Mwana kondoo wa pasaka. Kuongeza zaidi kitu kwa lengo la kusisitiza, au kukuza zaidi ya uhalisia. “ jicho lako la kuume likikukosesha ling’oe ulitupe mbali nawe . . . ” (Mt. 5.29). Vitu visivyo na uhai vinaongelewa kana kwamba ni watu, au kana kwamba vina uhai “ bahari iliona ikakimbia . . . ” (Zab. 114.3). Kugeuza kutoka kwa wasikilizaji wa muda huo ili kumzungumzia kitu au mtu ambaye hayupo hapo au ni wa kufikirika. “ Ee, upanga wa Bwana, siku ngapi zitapita kabla hujatulia? ” (Yer. 47.6). Pale ambapo kitu kizima kinatajwa kama sehemu tu ya hicho au sehemu ndogo ya kitu inatajwa kama ni kitu kizima, mtu mmoja darasa zima na kinyume chake. “tulipata watu [katika tafsiri ya KJV, souls yaani nafsi ] mia mbili na sabini na sita . . .” Katika Mdo 27.37, pale ambapo nafsi inatumika badala ya ajili ya mtu katika ukamilifu wake.
KEJELI/KINAYA ( Eiron = mzungumzaji anayeongea kinyume) TAASHIRA ( Meta + onoma = kubadilika kwa jina) CHUKU ( Huper + bole ) = kuongeza zaidi ya uhalisia TASHIHISI (kujifanya kama mtu)
RITIFAA ( apo + strepho = kugeuza kutoka)
TANIABA ( Sun + ekdechomai = kupokea na kuhusiana na)
Tashbihi
Kwanza, hebu tulinganishe tashbihi na sitiari. Waefeso 5:22-27 ni tashbihi, kuweka ulinganifu rasmi kati ya Kristo na Kanisa katika upande mmoja na waume na wake upande mwingine. Maneno “kama vile . . . ndiyo ilivyo” au “vivyo hivyo” yanaweka hili wazi zaidi. Na mfano huu unakuza shauku yetu na kuimarisha mahusiano katika ndoa, na hasa kama tunaliona katika hali yake ya mchanganuo, kama hivi:
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker