Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 2 5 7
K U T A F S I R I B I B L I A
Tamathali za Semi (muendelezo)
KAMA ilivyo kwa KRISTO NA KANISA
NDIVYO ilivyo kwa WAUME NA WAKE ZAO WAUME, WAPENDENI WAKE zenu kama KRISTO ALIVYOLIPENDA KANISA (Efe. 5.25) KWAMBA mume anaweza kumtakasa mkewe. Yaani ili aweze KUHUSIKA KATIKA MAISHA YAKE, na kuwa msaidizi wake, n.k a) kuonyesha utu na maisha yake mwenyewe katika Kristo. b) kutumia vipawa vyake katika huduma ya kiroho. c) awe mtawala wa nyumba , katika yote ambayo yana maana kwa muwe wake na watoto. KWAMBA mume anatakiwa kutafuta furaha ya mkewe na kumfurahia, yaani ili aweze kufurahia uzuri na utukufu wa utoshelevu wa uanawake wa mkewe huku anaendelea kufanya wajibu wake yeye kama kichwa akimuongoza mkewe katika uongozi wenye upendo kuelekea katika utimilifu wa mwisho. KWAMBA mume awe mwaminifu, adumu katika huo, yaani ili kujitoa kwake kuwe imara na kwa kudumu, licha ya matatizo. Waume wanatakiwa kutunza mawasiliano endelevu, wakikumbuka kwamba upendo huwa unatafuta njia ya KUWASILIANA, na ni kwa jitihada zake Mwanaume kama kweli anataka kupenda kama vile KRISTO ALIVYOPENDA.
KRISTO ALILIPENDA KANISA na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake (Efe. 5.25) “ KWAMBA, aweze kulitakasa ” (Efe. 5.26) yaani, tuweze kuwekwa katika matumizi yaliyokusudiwa na yeye alipotuumba: a) Kama udhihirisho wa MAISHA na TABIA yake mwenyewe . b) Kutimiza wito wetu, kufurahia huduma ambazo Mungu ametupa. c) na mengine mengi (ongeza yaliyobaki) “apate kujiletea Kanisa tukufu” (Efe. 5.27) yaani ili kwamba aweze kufurahia faida zinazotokana na upendo wake usio na ubinafsi katika kumfurahia bibi harusi wake. Na kutuongoza katika utimilifu wa uanaume wetu na uanawake wetu katika upendo wake. “BALI liwe takatifu na lisilo na mawaa” (Efe. 5.27). Yaani, kazi yake kwetu iweze kuendelea mpaka ukamilifu wake, na ili tuwe wake kikamilifu. “ Ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika Neno; ” (Efe. 5.26) kutegemeana na MAWASILIANO ambayo moyo wake wenye upendo umeyaanzisha-kutuweka karibu, na kufurahia uhusiano wa upendo wetu kila mmoja kwa mwenzake.
Sitiari
Kinyume chake, sitiari si ya moja kwa moja sana. Inawasilisha namna yake zaidi kwa njia ya kudokeza. Katika semi, “ Ninyi ni chumvi ya dunia . . .” (Mt. 5:13) na “Ninyi ni nuru ya ulimwengu ” (Mt. 5:14), Bwana wetu Yesu Kristo anazikuza sitiari,
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker