Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
2 5 8 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Tamathali za Semi (muendelezo)
ili kuwasilisha ukweli kwa njia ya picha kuhusu jukumu lenye athari kubwa ambalo wakristo wanatakiwa kulitekeleza katika kuuathiri ulimwengu. Katika siku hizo, chumvi ilikuwa njia muhimu zaidi ya kuzuia nyama na samaki kuharibika, kwa hiyo mfano huo haujakosewa kwa wale waliokuwa wanamsikiliza Yesu. Nuru, katika wakati wowote inatusaidia kufanya kazi kwa kiwango chochote cha ujasiri. Inafukuza giza. Tunapokuwa hatuoni, hapo tunakuwa katika shida. Maneno “chumvi” Na “nuru” Yanatumika kama vidokezi vya ulinganifu. Sitiari hizi huzungumza kwa nguvu ya kupenya, ingawa huwa sio za wazi kwa asili yake. Matumizi ya kejeli kama tamathali za semi, japokuwa zina ukakasi kidogo, mara nyingi zina upande wa ucheshi pia. Bwana wetu alikuwa anatumia pande hizo zote pale aliposema, “. . . Unawezaje kumwambia ndugu yako, ndugu yangu, niache nikitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako, nawe huangalii boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe?” (Luka 6:42). Katika 1 Wakorintho 4:8, Mtume Paulo anatumia kejeli kwa nguvu kubwa, “Mmekwisha kushiba, mmekwisha kupata utajiri, mmemiliki pasipo sisi. Naam, laiti mngemiliki, ili sisi nasi tumiliki pamoja nanyi!” Tunapoendelea kusoma, Paulo anaendela kutofautisha hali za mitume kama watu wa mwisho—sio wa kwanza, kama waajabu kwa ulimwengu, bali kama wapumbavu, kisha anatumia tena kejeli, “Sisi tu wapumbavu kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye akili katika Kristo; sisi tu dhaifu, lakini ninyi mna nguvu; ninyi mna utukufu, lakini sisi hatupati heshima” (1 Kor. 4:10). Unaweza kufiki namna ambavyo wakristo wa Korintho walijisikia aibu kwa namna ambavyo hawakuweka thamani katika vile vinavyostahili? Ni kwa namna gani Neno hili lenye makali la kejeli linaweza kuwa liliangusha kiburi chao kikubwa katika watu? Tunaweza kupitia upya namna yetu ya kutoa thamani kwenye vitu, leo, na kugundua misingi pekee ya kujivuna?—Yaani, Bwana Yesu na uzima wake ndani yetu. Kejeli/Kinaya
Taashira
Kisha kuna taashira (kubadilika kwa jina). Alipokuwa anaongea na mafarisayo kuhusiana na Herode, Kristo alisema “nendeni mkamwambie yule mbweha. . .” ( Luka 13:32) na kwa Neno moja alitoa sifa ya Mfalme mjinga. Na, “njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe. . .” (Mit. 12:15) ambapo macho
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker