Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 3 0 9
K U T A F S I R I B I B L I A
Uvuvio wa Biblia Chanzo na Mamlaka ya Biblia
MAELEZO YA MKUFUNZI 1
Karibu katika Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 1, Uvuvio wa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia . Shabaha ya jumla ya moduli ya Tafsiri ya Biblia ni kuwawezesha wanafunzi wako kupata maarifa yanayohitajika ili kuwa watafsiri wenye ufanisi wa Neno la Mungu. Shabaha ya moduli hii ni ushirikiano wa mtafsiri wa Biblia na Roho Mtakatifu, ambaye kiukweli ndiye chanzo cha uvuvio na kungaziwa kwa Maandiko yake. Hakuna yeyote anaweza kuyaelewa Maandiko kikamilifu bila msaada na uongozi wa Roho Mtakatifu (1 Kor. 2.9-16). Bado, kama watenda kazi wa kiume au wakike wasio na sababu ya kutahayari lakini kama hao watafutao kukubaliwa na Mungu, tunawiwa kubeba wajibu wa kulitumia kwa halali Neno la kweli, au kama tafsiri nyingi zinavyosema, kushika Maandiko kwa usahihi (2 Tim. 2.15). Kwa kupitia bidii yetu, mbinu zetu madhubuti, na zana pamoja na nyenzo ambazo wanaume na wanawake wenye vipawa ndani ya kanisa wametupa sisi, tunaweza kuutimiza wajibu wetu, na hivyo kuweza kutafsiri Neno la Mungu kwa ajili ya chakula chetu wenyewe na kwa wale wanaotusikiliza (1 Tim. 4.15-16). Katika somo hili tunalenga hasa katika Uvuvio wa Maandiko , msingi na chimbuko katika uongozi na maelekezo ya Roho Mtakatifu. Kupita utendaji wake mkuu na neema yake, Roho Mtakatifu aliwaongoza waandishi wa Biblia kuandika maneno, mawazo, dhana na yote aliyotamani yaandikwe, na kwa kila namna alitumia miundo yao, misamiati yao na matumizi yao ya lugha ili kutoa ujumbe sahihi ambao Mungu aliukusudia. Moyo wa ufasiri wowote wa Biblia ni tabia na uweza wake wa kimungu; hili, kutokana na ushahidi wa Biblia yenyewe, ni matokeo ya moja kwa moja ya utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Profesa Gerald Hawthorne kwa uangalifu na umakini anatoa maana ya uvuvio wa Roho Mtakatifu, akitoa maelezo kwa usahihi kuhusu uelewa wa Kanisa juu ya madai haya nyeti: Katika Agano la Kale kanuni ambayo manabii wa zamani walikuwa wanaitumia mara kwa mara kama utangulizi kwa ajili ya unabii wao iliokuwa ni, “asema Bwana” (Yer. 9.23, na kuendelea), “Bwana amesema” (Isa. 1.2, na kuendelea), “lisikieni Neno la Bwana” (Isa. 1.10, na kuendelea), “Neno la Bwana likanijia” (Ezek. 33.1, na kuendelea), au yanayo fanana na hayo. Utangulizi wa namna hiyo ulikuwa unakusudia kuwahakikishia hadhira kwamba ujumbe ulioenda kwao, ulioandikwa au kusemwa haukuanzishwa na nabii bali Mungu. Neno la nabii lilikuwa ni Neno la Mungu na lilitakiwa kupokelewa hivyo.
1 Page 15 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker