Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
3 1 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Katika Agano Jipya na Mababa wa Mwanzo wa Imani wamebadilisha kanuni hizi za Kale katika maeneo mengi na kuwa kanuni moja, “Roho Mtakatifu amesema,” Au Neno lolote la namna hiyo. Waandishi wa fasihi yetu walimuelewa Roho Mtakatifu kama ushawishi wa Mungu ulioenea katika maisha ya watu fulani, ukiwavuvia, ukithibisha ujumbe wao kwa nguvu yake kama maneno matakatifu, yenye mamlaka na ya mwisho. Tazama maoni ya Petro kwa wale wanafunzi 120 baada ya ufufuo na kuinuliwa kwa Yesu: “ndugu ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi” (Mdo 1.16). Maneno haya ya Petro yanatuonyesha wazi kile ambacho kiliaminiwa na watu wengi wa Kanisa la mwanzo kuhusiana na Agano la Kale kwa ujumla—Roho Mtakatifu alikuwa ndiye chanzo kikuu; Roho Mtakatifu alikuwa anaongea kupitia watu, kama Daudi, ili kwamba kile ambacho kitahifadhiwa katika Agano la Kale kiwe ni Neno la Mungu, Neno la Roho wa Mungu (tazama pia Mdo 4.25; 28.25; Ebr. 3.7; 9.8; 10.15; 1 Klem. 13.1; 16.2; 22.1; 45.2; linganisha. 8.1; Ban. 9.2; 10.2, 9; 14.2). Maoni ya mwandishi wa 2 Petro 1.21–22 katika eneo hili, japo kuwa andiko lenyewe ni gumu kulitafsiri : “maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi wa Mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu , wakiongozwa na Roho Mtakatifu. Tazama pia kwenye toleo la NIV). Hata hivyo mtu mmoja hatimaye anatafsiri mstari huu, ujumbe wake umeeleweka: “sehemu pekee ambapo mwandishi wa 2 Petro anaonekana kupakataa ni dhana ya kwamba manabii wenyewe ndio walikuwa chanzo cha jumbe zao. Katika kuweka sawa hoja hii anathibitisha kwamba Roho Mtakatifu ndiye alikuwa chanzo cha unabii wao, akiwawezesha kuongea kama wasemaji kwa niaba ya Mungu” (Bauckham, 234; linganisha. Philo Rer. Div. Her. 259; Philo Vit. Mos. 1.281, 286). Ushuhuda wa pamoja wa Kanisa la kwanza kuhusu Agano la Kale ni kwamba lilikuwa ni Neno la Mungu, kwa sababu wale watu walioruhusiwa kuongea au kuandika ujumbe wake, waliongea au kuandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu na hivyo waliongea na kuandika wakiongozwa na Mungu. Mungu aliongea na watu wake kupitia Daudi, Isaya, Yeremia, na wengine kwa njia ya Roho Mtakatifu (Mdo 4.25). Lakini vipi kuhusu Agano Jipya? Luka alitambua kwamba Roho Mtakatifu bado alikuwa anaongea kipindi cha mitume (Mdo 13.2; 20.23), na mwandishi wa waebrania hasemi tu kwamba hema na huduma za kikuhani zilikuwa zimevuviwa bali pia anasema kwamba Roho Mtakatifu alikuwa bado anaongea—katika siku zake—na anaonyesha kwamba njia ya kuingia patakatifu ingekuwa haijadhihirishwa bado kama hema ya kwanza ingekuwa bado imesimama (Ebr 9.8). Klementi anaonekana kuwa sahihi zaidi kwamba mitume
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker