Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 3 1 1

K U T A F S I R I B I B L I A

walishiriki uvuvio uleule kama wa manabii wa Agano la Kale. Aliandika kwamba wao “wakiwa wamekwisha kupokea amri yao, na kuhakikishwa kwa ufufuo wa Bwana wetu Yesu Kristo . . . Waliendelea wakiwa na uhakika kwamba Roho Mtakatifu anatoa uwezo wa kuhubiri habari njema ” (1 klem. 42.3). Tena, kwa habari ya Paulo anaandika, “kwa uvuvio wa kweli (ep’ aletheias pneumatikos) aliwaamuru kuhusiana na yeye mwenyewe na Kefa na Apolo” (1 klem. 47.3). Kutokana na Maandiko haya machache inawezekana kuamini kwamba Roho alikuwa bado anaongea wakati wa kipindi cha mitume, akiwavuvia wale waliojiandaa kuwa sauti ya Mungu ulimwenguni. ~ Gerald F. Hawthorne. “The Holy Spirit.” Dictionary of The Later New Testament and Its Developments (Electronic ed.). R. P. Martin, Ed. Downers Grove: Intervarsity Press, 2000. Katika moduli hii yote na somo hili tunataka kusisitiza ukuu na nguvu ya Roho Mtakatifu ya kutuekeza, kutuongoza katika kutumia kwetu Maandiko kwa bidii, kwakuwa kwa kweli, yeye ndiye mwandishi na chanzo. Malengo yaliyopo hapa chini yana ashiria kweli hii, na itakuwa ni muhimu kwako pia kuendelea kusisitiza kweli hii katika moduli yote. Yaseme malengo waziwazi na uyarudie mara kwa mara. Unapoendelea kuyasisitiza katika somo lote, katikati ya mijadala, katika majibu ya majaribio na mitihani, na wakati wote unapochangamana na wanafunzi utakazia kile ambacho yumkini ndio dhana ya msingi katika fundisho lote: Kwamba uongozi na upako wa Roho Mtakatifu ni kigezo cha muhimu sana katika kukuza uwezo wetu wa kulisikiliza Neno la Mungu na kulitendea kazi kwa uaminifu katika maisha yetu na huduma zetu. Kiukweli, kwa kadri unavyoweza kuendelea kuweka msisitizo kuhusu malengo husika katika muda wote wa kipindi, ndivyo unavyozidi kuongeza uwezekano wa wao kuelewa uzito wa malengo haya. Moduli za mtaala wa Capstone zimetengenezwa kwa kuonyeha malengo ya somo na ya kujifunza katika kila hatua ya somo. Haya sio kwa ajili ya kuyataja tu na kuyapuuzia; badala yake, malengo haya yanawakilisha kiini cha somo katika moduli. Uwezo wako wa kuhusiana nayo katika mchakato wote wa kujifunza ndio utakuwa tofauti kati ya kumaliza kujifunza yaliyoandikwa na kuwaelekeza wanafunzi wako katika kweli za msingi zilizopo katika mbinu zitumikazo na faida za ufasiri wa Biblia wenye tija na ufasaha.

 2 Page 15 Malengo ya Somo

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker