Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

3 1 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Hivyo ni muhimu, kwakuwa wewe ni mkufunzi, uyazoee malengo ya somo vizuri kila mwanzo wa somo la Capstone . Hayo ndio yanaongoza na kuweka sawa maudhui ya somo, kutoka kwenye kipengele cha video mpaka kwenye mijadala na mitihani. Machapisho yote yanalenga na yameunganishwa ili kutimiza malengo haya. Hivyo tafadhali usisite kusisitiza malengo haya wakati wowote wa kufundisha kwako, lakini mara zote fanya hivyo unavyoanza kipindi. Vuta umakini wa wanafunzi kwenye malengo, kwa sababu kwa hali halisi, huu ndio moyo wa lengo lako la elimu hiyo katika kipindi darasani katika somo hili. Kila kinachojadiliwa na kufanyika kinatakiwa kurejea kwenye malengo. Tafuta njia ya kuweka mkazo kwa malengo haya kila wakati, ili kuwaimarisha na uyarudierudie unapoendelea. Ibada hii inalenga kwenye kweli (ukweli) na uaminifu wa Mungu katika Agano lake kama ilivyoonyeshwa kwenye Neno lake na hakika yake. Kwa sababu Mungu wetu, Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ni wa kweli, tunaweza kulitegemea Neno lake. Ni muhimu kutokutenganisha madai ya Biblia kuhusu Maandiko na asili ya Mungu mwenyewe. Neno la Mungu ni amini na kweli kwa sababu Mungu mwenyewe ni amini na kweli. Sawasawa na ushuhuda wa kweli na amini (Ufu. 19.11), hukumu zake kamilifu ni za kweli (Ufu. 19.2) pamoja na maneno ya ushuhuda kuhusu matendo yake na makususdi yake (Ufu. 21.5; 22.6). Kuyaelewa Maandiko ni kujua kwamba katika uungu wa Mungu hakuna hata chembe ya unafiki, uongo, kutofautiana, au ukafiri uliomo ndani yake. Neno lake ni kweli kwasababu yeye ni mwaminifu na wa kweli, Bwana wa wote. Ufahamu huu wa kweli kamili ya Mungu ndio sababu kwanini tunahamu ya kujifunza Neno lake, na kwanini linaweza kutufanya wenye hekima kwa ajili ya wokovu katika Kristo. Ahadi zake zinastahili kujifunza kwazo na ni amini kwasababu aliyeziahidi ni mwaminifu (Ebr. 10.23). Tunaweza kukiri dhambi zetu kwa ujasiri kulinganan na Neno lake, kwasababu yeye ni mwaminifu kutusamehe dhambi zetu (1 Yohana 1.9). Tuna unakika wa kuja kwa Bwana wetu na utukufu ujao, kwasababu Neno la Mungu mwaminifu limetuhakikishia kwamba Mwanaye atakuja, na tutabadilishwa kabisa yeye akirudi (1 The. 5.23-24). Ili kuona uhusiano huu wa nafsi ya Mungu na umilele wake, Neno lenye uaminifu ndio ufunguo wa kila kiwango cha maisha yetu ya kikristo: Mungu mwaminifu atatupa ushindi dhidi ya yule mwovu (2 The. 3.3), atatuokoa katika tukio lolote la kishawishi na jaribu (1 Kor. 10.13), na kamwe hatatuacha, hata ule wakati usiofaa ambao

 3 Page 16 Ibada

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker