Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 3 1 3

K U T A F S I R I B I B L I A

tunaonekana kupoteza imani kwake, kwa sababu kwa njia yoyote yeye anabaki kuwa mwaminifu, kwa sababu hawezi kamwe kuikana asili yake kamilifu na ya uaminifu. (2 Tim. 2.13). Sisitiza katika somo lote hili kwamba imani yetu katika Maandiko kimsingi ni ujasiri tulionao katika tabia yake yeye aliyelivuvia Neno hilo, na amelitunza liwe takatifu kwa ajili ya imani yetu na utii wetu, hakuna ahadi yoyote ya Mungu ambayo itashindwa kutimia (1 Wafalme 8.56), kwa kuwa kila mmoja anakamilishwa na uaminifu wa Mungu ambao aliupanga tangu mwanzo (Isa. 25.1). Wahimize wanafunzi watambue uaminifu huu kupitia kujifunza kwao na kutafakari kwao juu ya Neno la Mungu. Maandiko ni udhihirisho wa uaminifu wa milele wa Mungu ambao haujawahi na kamwe hauwezi kupotoshwa. Tunalishikilia Neno lake kwa sababu yeye aliyelitoa yuko mbali na hila, uongo, au aina yoyote ya kutokuwa mkweli. Kwa karne nyingi za ukiri, uthibitisho na matamko, Mungu wetu hajawahi hata mara moja kuwa katika kosa kuhusiana na ahadi yake au Neno lake. Kama Bwana wetu alivyosema, Maandiko yako imara yaani hayawezi kamwe kutanguliwa (Yohana 10.35). Watie moyo wanafunzi kuendelea kushikilia Neno kama lilivyo sawasawa na Mungu anavyotangaza. Huu ndio mwanzo wa kutembea kwa imani (2 Kor. 5.7), ambao pasipo hiyo Mungu hawezi kupendezwa kwa namna yoyote ile (Ebr. 11.6). Neno la Mungu litatimiza kile ambacho Mungu anakusudia, ahadi zake kamwe haziwezi kuwa tofauti, na mafundisho yake ni kweli kamilifu. Kwa sababu anajua yote, ukiri wake ni kweli isiyobadilika kamwe. Kwasababu yeye ni mwaminifu, ahadi zake zitatimia. Tegemea hili; hakuna chochote kitakacho chipuka au kutokea kwetu au ulimwenguni ambacho kitamfanya Mungu ashangae, au ambacho bado hakijajulikana katika kusudi lake na ufalme wake. Neno lake litatimiza kile ambacho anakusudia likifanye, na katika msingi huu, tunajenga imani yetu. Kujenga Daraja katika somo kunalenga katika uhusiano kati ya njia, mbinu za kisomi, zana, na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu . Mara nyingi vitabu vinavyoelezea somo hilo ama vinazungumzia utendaji wa Roho Mtakatifu kama nadharia tu na kusisitiza zaidi juu ya mbinu zinazotumika, au vinadunisha umuhimu wa mbinu na kusisitiza zaidi utendaji kazi wa Roho katika ufasiri wote fasaha ya Biblia. Utahitaji kuwasadia wanafunzi wako kuelewa uhusiano kati ya hivyo viwili na tafuta

 4 Page 19 Kujenga Daraja

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker