Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
3 1 4 /
K U T A F S I R I B I B L I A
kueleweka kwa aina ya njia ambayo inafanya vizuri bila kuondoa umuhimu wa nyingine.
Maswali haya yametengenezwa ili kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa malengo ya msingi na kweli zilizoonyeshwa katika kipengele cha kwanza cha video. Utatakiwa kupima muda wako vizuri, hata kama wanafunzi wametatizika kidogo kuhusiana na dhana fulani na wanahitaji kujadili maana zake kwa marefu kidogo. Tenga muda wa kutosha kwa ajili ya mambo muhimu, na bado uwe na muda wa kutosha kwa ajili ya mapumziko kabla kipengele kinachofuata cha video hakijaanza. Zilizo orodheshwa hapa chini ni kweli za msingi zilizoandikwa katika sentensi ambazo wanafunzi wanatakiwa wawe wamepokea kutoka katika somo hili, hizo ni kutoka kwenye kipengele cha video pamoja na mjadala uliouongoza pamoja nao. Hakikisha kwamba dhana hizi zimefafanuliwa vizuri na zimezingatiwa kwa umakini, kwakuwa kazi zao za mazoezi, na mitihani, zitachukuliwa moja kwa moja toka katika kweli hizi. Ili kufanya yale waliyojifunza yawe ya kwao, wanafunzi wanatakiwa kufundishwa kufikiri kuhusu umuhimu na utendeaji kazi wa kweli hizi katika maisha yao wenyewe. Kuweka uhusiano kati ya maswali yao pamoja na hali zao wanazopitia ni ufunguo kwa dhana hizi kuwabadilisha. Kwahivyo kazi yako itakuwa, kuwasaidia wanafunzi wako katika sehemu hii ya somo kufikiri kuhusu hali zao halisi, huku wakitafakari maana ya somo. Unaweza kutaka kutengeneza baadhi ya maswali, au kuyatumia yale yaliyoonyeshwa hapa chini ili “kuibua shauku” yao kwa ajili ya somo. Tunachokitafuta hapa sio shughuli nyingi pamoja na maswali yaliyo na ukweli, bali tunafanya uchunguzi wa maana za kweli hizo juu ya maisha yao wenyewe. Nini cha muhimu basi, sio tu kwamba wajibu maswali yaliyoonyeshwa hapa chini, bali waweze kuainisha masuala mbalimbali yanayowahusu, maswali, na mawazo ambayo yanatoka moja kwa moja kutoka kwenye uzoefu wao, na yanahusiana na maisha na huduma zao.
5 Page 32 Maswali kwa
Wanafunzi na Majibu
6 Page 50 Muhtasari wa Dhana za Kuu
7 Page 53
Kutendea kazi somo na matokeo yake kwa mwanafunzi
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker