Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 3 1 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Usisite kutumia muda mwingi zaidi katika maswali ambayo yanajitokeza kutoka kwenye video, au jambo fulani maalum ambalo ni muhimu katika muktadha wa huduma yao kwa sasa. Dhumuni la sehemu hii ni wewe kuwawezesha wao wafikiri kwa makini na kitheolojia kuhusiana na maisha yao na muktadha wa huduma. Nasisitiza, maswali hapa chini yametolewa kama mwongozo na vitangulizi tu, na yasichukuliwe kama hayo ndio ya lazima zaidi ya mengine. Chagua miongoni mwa hayo, au uje na ya kwako mwenyewe. Jambo la msingi sasa ni umuhimu, kwenye muktadha wao na maswali yao. Masomo rejea haya yametengenezwa ili kuwasaidia wanafunzi, kutendea kazi uelewa wao juu ya dhana na kanuni kwenye maswali na hali halisi ambazo eidha zimeshatokea au zinazoweza kutokea. Kuwasaidia wanafunzi kujifunza na kuwa wabunifu katika kuzitumia kweli kwenye hali fulani inayohitaji kushughulikiwa; lengo la ujuzi mtu aliojifunza hapa ni kutendea kazi hekima katika mazingira husika. Hekima inatutaka kwamba tutumie maarifa ya kweli katika hali husika kwa namna sahihi na inayotosheleza katika kutoa suluhisho la tatizo, au kuwaimarisha wale wanaohusika. Katika hili, masomo rejea haya ni “muhimu sana” Kwa ajili ya uwezo wao mkubwa wa kutumia kweli katika hali halisi za maisha. Mazoezi yanatolewa kwa wanafunzi ili kuwafanya wajiandae kwa ajili ya mijadala na maelezo ya kuyasoma kwa ajili ya kipindi kinachofuata, sambamba na kupitia maelezo hayo kwa ajili ya chemsha bondo, mazoezi yanayohusiana na kazi zitolewazo katika kipindi kilichopo. Mara zote hakikisha wanafunzi wanaelewa kile wanachotakiwa kufanya katika mazoezi yao kwa ajili ya kipindi kinachofuata, na hasa elezea wajibu wao kwa kuandika sehemu. Sambamba na hilo, muhtasari ulioandikwa(dibaji) haujalenga kuwa kazi kubwa kwa wanafunzi; lengo ni kwamba wasome maelezo vizuri wawezavyo na waandike sentensi chache kuonyesha nini kina maanishwa. Huu ni ujuzi wa makini wa kisomi kwa wanafunzi wako kujifunza, hivyo hakikisha unawahimiza katika mchakato huu. Bila shaka, kwa wale wanafunzi ambao wataona hii kuwa ni ngumu kwao, wahakikishie umuhimu wa kile kazi hii inakilenga, na usisitize uhitaji wa wao kupambana na dhana za maelezo haya, na kwa ufupi waonyeshe muhtasari kwa

 8 Page 54 Uchunguzi Kifani

 9 Page 58 Kazi

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker