Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 3 1 9
K U T A F S I R I B I B L I A
Biblia na kutafsiri vizuri zaidi hadithi za Biblia? Kutumia maarifa kwa namna hii kunaweza kutusaidia kutambua maana ya andiko katika hali ya upana zaidi. Tafadhali zingatia tena kwamba malengo yameeleza kwa wazi kweli hizi. Kama kawaida, wajibu wako kama Mkufunzi ni kusisitiza dhana hizi katika somo zima, hususani katika mijadala na pale unapochangamana na wanafunzi. Unavyozidi kuweka msisitizo kwenye malengo katika kipindi kizima darasani, ndivyo unazidi kuongeza uwezekano kwa wanafunzi kuelewa na kutambua uzito wa malengo haya. Ibada hii inalenga katika maandalizi ya moyo ambayo ni muhimu ili kupata uelewa wote unaotokana na mbinu muhimu zitumikazo katika ufasiri wa Neno la Mungu. Kiukweli Maandiko ni kitabu cha fasihi, lakini tofauti pekee inayofanya kisiwe kama vitabu vingine ni kwamba kinaweza kubadilisha nafsi ya mwanafunzi anayekiendea kwa namna ya kufanya mafundisho yake kuwa ni kukutana na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo katika nguvu ya Roho Mtakatifu . Lengo la kujifunza Biblia sio ili tu kutatua udadisi au kupata dondoo kwa ajili ya mijadala au mabishano; Neno, kwa habari ya Ezra, lilikuwa kwa ajili ya kurekebisha maisha yake na nguvu ya kubadilisha maisha ambayo ingemsaidia kuhusiana na Mungu kwa namna ambayo ilimfanya awe chombo na kifaa kwa ajili yake. Mwandishi Paul Karleen ameongea kwa ufasaha kuhusu kiwango cha Neno la Mungu na namna linavyoweza kubadilisha maisha ambayo kwa kweli lazima lilete athari chanya katika maandalizi binafsi na utayari wa mwanafunzi yeyote wa Biblia aliyemaanisha: Moja kati ya makosa makubwa ambayo wanafunzi wa Biblia wanaweza kufanya ni kufikiria kwamba juhudi zao pekee ndizo zinaweza kuamua kile ambacho watakifaidi kutoka kwenye Maandiko. Mtunzi wa kiungu wa Biblia huyo ndiye mtafsiri wa mwisho. Mwamini anaweza kuteigemea kweli ya 1 Kor. 2.12: “lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua yale tuliyokirimiwa na Mungu.” Wale wanaomfahamu Yesu Kristo kama Mwokozi wana Roho Mtakatifu ndani yao anayewaangazia nuru katika Maandiko. Kuzaliwa mara ya pili ni kigezo cha kwanza cha kufanya Biblia ieleweke.
2 Page 62 Ibada
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker