Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
3 2 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
Pia, kwasababu Mungu anaongea nasi kwa njia ya Neno lake, lazima tuzingatie kila sehemu tunayoisoma au kujifunza katika Neno kana kwamba ni kukutana na kumsikia Mungu mwenyewe. Kama vile unavyokuwa na shauku kwamba Mungu afuinue kweli za kiungu kwako, vivyo hivyo inabidi uwe tayari kuachilia hali yako ya kiroho iwe wazi mbele za Mungu unapokifungua Kitabu. Na unapozidi kulielewa vizuri na kulitendea kazi katika maisha yako, ndivyo linavyozidi kukuonyesha mahitaji ya kiroho uliyonayo. Ni moyo uliopondeka ndio unaweza kupata malisho zaidi kutoka katika Maandiko. Ingawa Biblia ina mambo ya kutosha tu kutia changamoto watu wenye ufahamu mkubwa kabisa katika kujifunza kwa maisha yao yote (na bado hawawezi kumaliza maudhui yake!) ni utayari wa mtu binafsi na utendeaji kazi wa kweli zake ndivyo ambavyo vinalengwa hapa. Mwandishi Vance Havner alilielelewa hili aliposema: Akiba ya Neno la Mungu haikuwekwa kwa ajili ya tafakuri ya kawaida tu, wala hata sio kwa ajili ya kusoma tu bali kwa ajili ya kuwa kuleta utajiri. Sio mkusanyiko wa mithali za kawaida na mafundisho mazuri kwa wanadamu ili kuhamasika na kunukuu wanapotunga mashairi. Ni chakula kwa ajili ya nafsi, ni nyenzo kwa ajili ya roho, ni hazina kwa ajili ya mtu wa ndani. Kila bidhaa inayopatikana katika kila ukurasa ni ya kwetu, na hatuna shughuli yoyote ya kufanya nazo ila ni kuziendea na kurudi na utajiri kutoka katika hizo. ~ Paul Karleen. The Handbook to Bible Study . (Electronic ed.). New York: Oxford University Press, 1987. Kwa kweli, Biblia haijakusudiwa kuchunguzwa tu juu juu, kana kwamba unaweza tu kusoma ujumbe wake na kisha kwenda zako. Badala yake, ili tafsiri ya Biblia iweze kutubadilisha, lazima tuweze kuiona kama ndugu Havner alivyopendekeza: Kama “chakula kwa ajili ya nafsi zetu, nyenzo za na kwa ajili ya roho, hazina kwa ajili ya mtu wetu wa ndani” Wape changamoto wanafunzi wako ili kufikia hali ya kuwa makini, kuwa na kiasi na shauku katika maono yao kuhusiana na Neno ambalo Ezra alilishikilia, na labda Roho Mtakatifu atakuwa wa neema sana kwetu na kutupa aina hiyo hiyo ya matokeo kama aliyokuwa nayo kwa watu wa Mungu, kwa ajili ya utukufu wake.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker