Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 3 2 3
K U T A F S I R I B I B L I A
Fasihi ya Biblia Kutafsiri Tanzu za Biblia
MAELEZO YA MKUFUNZI 3
Karibu kwenye Mwongozo wa Mkufunzi kwa ajili ya Somo la 3, Fasihi ya Biblia: Kutafsiri Tanzu za Biblia . Shabaha ya jumla ya somo hili ni kuelewa umuhimu wa kutumia tanzu katika kutafsiri Biblia. Hata katika usomaji wa harakaharaka wa Biblia, mara moja tuna ona utofauti wa maandiko yaliyozalishwa katika maandishi kipindi cha ulimwengu wa Kale. Utofauti huu au tanzu hizi zinajumuisha upana wa mada, miundo na aina za fasihi. Kuhusiana na masuala hayo, tunapata maandishi kuhusu mada mbalimbali kama ufanyaji wa biashara, mazingaombwe, unajimu, hisabati, dini, sheria na utabibu. Katika upana wa maandishi ya kale tunapata pia maandishi kuhusu kosmolojia, hekaya, historia za kitaifa, na maono ya kidini. Mtu anaweza kugundua hadithi, nyimbo za mapenzi, mashairi, nyimbo za tenzi, mafumbo, nyaraka, na historia za watawala wa falme. Vilevile tunapata kazi za kiushairi, maandishi kuhusu hekima, hoja za kihistoria, na maandishi ya kinabii. Kwa kweli watu wale wakale hawakuamini kwamba “ukubwa mmoja unatosha kwa maumbo yote ” katika masuala ya mawasiliano; somo la aina na utofauti wa maandishi mbalimbali katika Maandiko ni kipengele cha muhimu sana katika kuelewa maana yake na umuhimu wake kwa leo. Fasihi ya Biblia ni aina gani has aya tanzu? Mwandishi na mwanatheolojia, Profesa Larry W. Hurtado anaeleza katika kamusi ya Dictionary of Jesus and Gospels : Tanzu za fasihi ni mgawanyiko au aina ya fasihi kama vile wasifu au riwaya. Tanzu za kifasihi haziko sawa maeneo yote na kugawanywa kwa namna moja tu, hapana, lakini zimekuwa zikizalishwa na kubadilika kadri muda unavyokwenda, na kwasababu hiyo tanzu moja ambayo ni maarufu katika zama au utamaduni fulani inaweza kutofahamika kabisa na utamaduni mwingine. Hata kama tanzu, kama za wasifu inatokea katika nyakati au utamaduni zaidi ya mmoja, bado tabia mahususi za tanzu hiyo zitatofautiana katika mpangilio wake. Katika kutafuta kutambua tanzu ya mwandishi, lazima tuzichunguze tanzu na kaida za fasihi ambazo zilizoeleka katika kipindi cha uandishi huo. Kwa mfano, swali la tanzu za injili lazima zifanyiwe kazi kwa kuchunguza sifa zake katika kulinganisha aina za fasihi katika mazingira ya nyakati za utawala wa Kigiriki na Kirumi (au angalau inayopatikana kwa waandishi). Tanzu zinatakiwa kufikiriwa kama mkusanyiko wa sifa au tabia. Uchambuzi wa kazi zinazohusiana na tanzu za fasihi unatakiwa uhusishe ulinganisho wa sifa zote za tanzu muhimu na zilizo na kazi katika suala husika.
1 Page 113 Utangulizi wa Somo
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker