Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

3 2 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Msisitizo katika sifa fulani tu mahususi za kazi ya fasihi unaweza kuleta hitimisho linalochanya na lisilo sahihi. Uandishi unaweza kuhusiana na aina fulani ya tanzu pale tu ambapo sifa zote za uandishi zinaweza kueleweka kwa kina kulingana na vigezo vya tanzu husika. Aina ya sifa na vigezo ambavyo vinazingatiwa katika kujaribu kutambua tanzu ya uandishi inajumuisha yafuatayo: Sifa za kisarufi (k.m., muundo, mtindo, mifumo, zana za uandishi) dhumuni la mwandishi, mchakato wa utunzi, mpangilio wa mwandishi, mpangilio wa matumizi yaliyokusudiwa, na maudhui. Kila msomaji analeta matarajio kwenye uandishi, ambayo yanatengeneza mchakato wa usomaji na kuboresha namna uandishi unavyoeleweka. Kuwa mzoefu wa tanzu za kiuandishi kunaruhusu uelewa wa uandishi kuongozwa na nuru ya sifa na malengo ambayo yanazipa tabia fulani tanzu hizo. Kama mwandishi akitaka kuandika kutokana na kanuni na sifa za tanzu husika, inaweza kuwa rahisi zaidi kutambua tanzu za uandishi. Lakini wakati fulani mambo sio mepesi sana, kwa mfano, kama mwandishi anatumia tanzu fulani kufanikisha dhumuni huku alikuwa hana uzoefu na tanzu hiyo kabla au kama mwandishi hafuati njia na kanuni za tanzu husika, inaweza kuwa ngumu zaidi kuainisha uandishi huo. Katika hali yoyote, kutambua tanzu ya uandishi inahitaji uchambuzi makini ambao lazima uzingatie ujuzi wa uandishi na muktadha wake wa kifasihi wa kijamii. ~ Larry W. Hurtado. “Genres.” Dictionary Of Jesus And The Gospels (Electronic ed.). J. B. Green, ed. Downers Grove, IL: Intervarsity Press, 1997. uk. 277. Lengo lako katika moduli hii ni kuwawezesha wanafunzi kufanya kama Profesa Hurtado anavyopendekeza, kuwa wazoefu wa tanzu husika ili uelewa wao wa kitabu katika suala husika uweze kuongozwa na maarifa hayo. Lengo ni kwamba wanafunzi waweze kuelewa aina ya fasihi wanayoisoma, ili waweze kuelewa baadhi ya sheria za msingi zinazohusiana na aina hiyo ya fasihi, na kisha waweze kufanya utafsiri kulingana na nuru ya kile ambacho wanakijua. Wakati ambapo inaweza kuchukua muda wote wa maisha kuelewa kikamilifu namna tanzu zinavyofanya kazi katika uhusiano wa fasihi ya Kale, mwanafunzi anaweza kufaidika mara moja kutokana na kuelewa baadhi ya kanuni za msingi za tanzu husika. Kama ilivyokuwa katika masomo yaliyopita, weka umakini wa karibu sana kwenye malengo, na lenga kwenye hayo kuwa kama ndio mafundisho hasa unapoendelea kulifundisha somo lako pamoja.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker