Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 3 2 5

K U T A F S I R I B I B L I A

Ibada hii inalenga katika kuona namna Mungu anavyotumia aina ya fasihi na mfumo wa fasihi wa mawasiliano yake kushughulikia utayari wa moyo wa watu wake. Fundisho hapa linathibitisha nguvu ya Biblia kama Neno la Mungu sio tu katika maudhui yake lakini pia katika mfumo wake. Tunaona kwamba Mungu alikuwa na nia ya wazi kabisa kutumia mfumo wa sitiari, taswira, mifano, ishara na hadithi kuelezea hali fulani ya moyo ya watu wake. Ujumbe haukutenganishwa na mfumo ambao ulikuja nao. Hii ni tofauti kubwa sana kutoka kwa kile ambacho Injili ya waprotestanti wanaihubiri leo. Huku wakiwa wamefundishwa kuongea maana vizuri ili kukwepa sitiari na taswira, kutumia hadithi kama tu kielelezo, na kukwepa kutumia lugha ya picha kwa gharama zote, matamko mengi yamepunguzwa mpaka kwenye madai matupu ya kitheolojia katika muhtasari uliomtupu zaidi pia. Kwa kweli, usemi huu ni sahihi kwamba, “tukiwa na njaa kwenye mimbari tutakuwa na maiti kwenye viti!” Mungu hayuko kinyume kiasi hicho na utumiaji wa sitiari, ndoto, mafumbo, taswira, nyimbo, mashairi na kila aina nyingine ya mawasiliano katika kuongea na moyo na nafsi za watu wake. Kwa wale ambao mioyo yao ilikuwa migumu na baridi, mifano au hadithi zilikuwa ni njia ya kuongeza ugumu wa mioyo yao; kwa wale ambao walitamani kumjua kwelikweli, ilikuwa ni mwaliko kwa kutafakari, kuuliza, kuchambua, na kufurahi. Kama mwelekeo wa kwanza wa mtu ni kupinga muziki wa jazi, kana kwamba ni ala zinazochanganya, usianze kuwalaumu wanamuziki wa jazi kwa muda huo huo. Unaweza kuwa na mtu ambaye hana ufahamu wa tanzu za jazi, na hivyo hawezi kutafsiri maana ya mashairi ya jazi kwasababu hana uzoefu na taratibu na namna muziki wa jazi unafanya kazi . Katika njia hiyohiyo, kabla mtu hajaweka maoni yake kuhusu sehemu fulani ya Biblia kama kama “inayoudhi na isiyovutia” Hapo usishikilie mara moja kwamba maoni yao ni ya kweli. Inaweza kuwa kwamba msomaji anahitaji kuboresha utayari wake ili kusikia na kuelewa aina hiyo ya fasihi. Tunachokitafuta hasa katika somo hili zima ni kutoa thamani ya kina kwa aina mbalimbali za ajabu za yale yaliyomo katika Neno la Mungu, na utayari na nia ya kuichunguza mantiki iliyopo nyuma yake,na hata kuwa mahiri katika kuyatambua na kuyatafsiri. Sisitiza kanuni hii katika somo zima, hasa kwa vile inavyohusiana na tanzu zilizomo katika Neno la Mungu.

 2 Page 114 Ibada

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker