Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

3 4 /

K U T A F S I R I B I B L I A

Kuvuviwa kwa Biblia: Chimbuko na Mamlaka ya Biblia. Sehemu ya 2: Kuvuviwa kwa Biblia na Uhakiki wa Kisasa wa Biblia

Mchungaji Dkt. Don L. Davis

Kwa mujibu wa madai ya Biblia yenyewe, imevuviwa na Mungu na inatambua vyanzo vyote viwili, kwa maana ya chanzo cha kimungu na cha kibinadamu, katika asili na mamlaka yake kama Neno halisi la Mungu Aliye Hai. Sisi wakristo tunaamini kwamba kwa kuwa Neno la Mungu limevuviwa na Mungu, halikuwa na makosa katika uandishi wake wa asili, na hivyo linawakilisha mamlaka kamili katika Kanisa la Mungu kwa habari ya kile tunachopaswa kuamini na kufanya. Uhakiki wa kisasa wa Biblia unajaribu kufuatilia asili ya maandiko kwa kuanzia na matukio ya awali yanayonenwa katika Biblia hadi simulizi halisi za matukio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vya kikanoni vya maandiko. Vipengele hivi vikuu vinajumuisha uhakiki wa muundo, chanzo, kiisimu, kimaandishi, kifasihi, kikanoni, uhakiki wa uandishi, na uhakiki wa kihistoria, pamoja na utafiti juu ya tafsiri. Bila kujali madai yanayotolewa na wasomi wengi leo, tunaweza kuwa na uhakika kwamba maandiko kwa kweli ni Neno la Mungu linaloishi na kudumu milele. Malengo yetu katika sehemu hii, Kuvuviwa kwa Biblia na Uhakiki wa Kisasa wa Biblia , ni kukuwezesha kuona kwamba: • Maandiko yanasema kwa uwazi na kwa ujasiri kwamba Neno la Mungu limevuviwa na Mungu, “limepuliziwa na Mungu,” kupitia nguvu na kazi ya RohoMtakatifu. Biblia ni kitabu kinachotokana na uandishi wa kibinadamu na uvuvio wa kimungu, hata hivyo hakuna andiko linalotokana na tafsiri yoyote ya matakwa ya mtu binafsi, bali waandishi “waliongozwa” na Roho Mtakatifu. • Kuna nadharia tano kuu za uvuvio zinazolenga kueleza jinsi Roho Mtakatifu alivyowaongoza kwa usahihi waandishi wa maandiko. Hizi ni pamoja na Nadharia ya Uvuvio wa Kiimla , Nadharia ya Uvuvio wa kihisia au uwezo wa asili, Nadharia ya Kuangaziwa, Nadharia ya uvuvio wa sehemu, na Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili . Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili ni imani ya kwamba maandiko yote ya Biblia, ikiwa ni pamoja na uchaguzi wa maneno aliyoyachagua mwandishi, ni matokeo ya uongozi na uchaguzi wa Mungu. • Uhakiki wa kisasa wa Biblia unajaribu kufuatilia asili ya maandiko kwa kuanzia na matukio ya awali yanayonenwa katika Biblia hadi simulizi halisi za matukio hayo yaliyorekodiwa katika vitabu vya kikanoni vya maandiko.

Muhtasari wa Sehemu ya 2

1

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker