Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

/ 3 3

K U T A F S I R I B I B L I A

3. Nini lengo la shughuli yoyote ya kutafsiri Biblia, kwa maneno mengine, tunapaswa kuzingatia nini tunapojifunza Biblia? “Kutumia kwa halali Neno la kweli” (2 Tim. 2:15) maana yake nini? 4. Dhanio ni nini, na ni “madhanio gani muhimu” ambayo Wakristo wamekuwa wakishikilia kuwa kweli siku zote kuhusu Biblia katika jitihada zao za kuifasiri ipasavyo? Kwa nini ni muhimu kujua madhanio hayo kama wafuasi waaminifu wa Kristo KABLA ya kujihusisha na mbinu mbalimbali za kutafuta kuelewa asili ya maandiko? 5. Kwa nini ni muhimu kuiona Biblia kama ufunuo endelevu ambao unafikia upeo wake katika ufunuo wa Yesu Kristo? Unafikiri kuna uhusiano gani kati ya Neno la Mungu lililoandikwa na Neno la Mungu katika nafsi , yaani Bwana wetu Yesu? Je, haya mawili yanahusianaje? 6. Eleza nafasi ya RohoMtakatifu katika uvuviowamaandiko na kuyaangazia maandiko katika ufasiri wa Biblia? 7. Mbinu ya Hatua Tatu ya Kutafsiri Bibliani nini, na ni kwa jinsi gani mbinu hii inalenga kuchukulia kwa uzito tofauti ya kihistoria na kiisimu (kifasihi) kati ya ulimwengu wa waandishi na ulimwengu wetu wa sasa? 8. Kwa nini haiwezekani kutafsiri Neno la Mungu bila kuwa na maandalizi moyo, akili, na nia ili kuliendea kama Mungu anavyokusudia? Je, hii ina maana kwamba tunapaswa kupuuza umuhimu wa kutumia mbinu na mikakati thabiti ya hemenetiki za kibiblia tunaposoma Neno la Mungu? 9. Ni baadhi ya majukumu gani tunayopaswa kuchukua tunapotafuta kutumia akili zetu kwa moyo wote katika kujifunza maandiko? Kwa nini utii ni muhimu sana katika kufahamu kikamilifu maana ya maandiko, na sio tu kusoma na kutafakari peke yake?

1

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker