Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

3 2 /

K U T A F S I R I B I B L I A

3. Tunakua kutoka kwenye hali ya uchanga kufikia utoto na hatimaye ukomavu kupitia utii thabiti wa Neno la Mungu.

a. 1 Petro 2:2

b. Waebrania 5:12-6.1

Hitimisho

1

» Ili kufasiri maandiko ipasavyo, ni lazima tuandae mioyo yetu, akili na nia zetu ili kujishughulisha na Neno la milele la Mungu Aliye Hai. » Kwa kuwa Biblia ni kitabu cha kimungu na cha kibinadamu, lazima tutegemee msaada wa Roho Mtakatifu ili kulielewa Neno la Mungu, na kuwa tayari kuruhusu Neno hilo kubadilisha maisha yetu kabla ya kuwashirikisha wengine.

Tafadhali chukua muda mwingi uwezavyo kujibu maswali haya na mengine yaliyoibuliwa na video. Hatupaswi kamwe kuliona somo la hemenetiki za kibiblia kama rundo la kanuni na mbinu ambazo zikitumiwa zitasababisha tupate mafunuo ya thamani yaliyomo katika maandiko. Badala yake, mada hii zima ni suala la kiroho, na ufasiri halisi wa kibiblia daima utahitaji maandalizi ya kiroho, msingi wa kimungu ambapo hautafuti tu kuelewa maandiko, bali kuyatendea kazi katika kila nyanja ya maisha yetu. Pitia maswali yafuatayo ambayo yanatoa muhtasari wa maarifa muhimu ya sehemu ya kwanza, huku ukizingatia kweli hizi katika ufahamu wako. Mara zote tumia Neno la Mungu kujenga msingi wa majibu yako. 1. Sayansi ya hemenetiki ni nini, nayo inahusu nini? Je, changamoto na lengo mahususi la hemenetiki ya Biblia ni lipi? 2. Tunamaanisha nini tuposema kwamba kimsingi Biblia lazima ichukuliwe kama kitabu cha kimungu na cha kibinadamu? Je, kuita Biblia kuwa kitabu cha kibinadamu kunapunguza au kupuuza madai yake kuwa ina asili ya kimungu? Eleza.

Sehemu ya 1

Maswali kwa wanafunzi na majibu

page 314  5

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker