Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 4 3
K U T A F S I R I B I B L I A
4. Ni ufunuo wa Kimungu ( maana yake linaweza tu kufasiriwa kwetu na Mungu mwenyewe, sio kwa tumia mawazo au uchambuzi wetu wenyewe ).
Kumbuka: Masomo ya Biblia ni jaribio la kugundua maana ya andiko katika muktadha wa jamii ya asili ya andiko husika, jinsi walivyoelewa tukio la kiufunuo, walivyoeneza habari zake, walivyolirekodi, na kulitafsiri kitheolojia.
D. Uhakiki wa muundo: kufuatilia mapokeo simulizi (hadithi, ripoti, shuhuda) zinazohusiana na matukio na maandishi.
1. Huchunguza mapokeo ya mdomo ya watu wa Mungu na Kanisa la kwanza.
1
2. Huiona Biblia kuwa zao la mapokeo ya wanadamu.
3. Uhakiki huu una kiwango cha chini sana cha uthibitisho.
4. Nguvu: msisitizo wake ni kwamba maandiko huenda yalikuwa na chimbuko katika simulizi kabla ya maandishi .
5. Udhaifu: hukisia na kubahatisha sana kuhusu namna jamii ya waaminio ilivyoeneza habari zake.
E. Uhakiki wa Chanzo: kugundua vyanzo vilivyoandikwa vilivyotumika katika uundaji wa vitabu.
1. Hulinganisha maandiko katika vitabu mbalimbali ili kuona kufanana na kutofautiana.
2. Huiona Biblia kuwa zao la mapokeo ya wanadamu.
3. Uhakiki huu kadhalika una kiwango cha chini sana cha uthibitisho.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker