Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 4 9
K U T A F S I R I B I B L I A
Maswali yafuatayo yametengenezwa kukusaidia kupitia yale uliyojifunza katika sehemu ya pili ya video. Suala la chimbuko, mamlaka, na uvuvio wa Biblia na ufasiri wa Biblia ndio kiini cha tafsiri zote za Biblia. Hatuwezi kuendelea kuelezea maana ya Hemenetiki mpaka tupate ufumbuzi kuhusiana na chimbuko la kimungu na la kibinadamu la Biblia. Uhakiki wa kisasa wa Biblia unalenga kuelezea uhusiano halisi uliyopo kati ya madai ya kimungu na kibinadamu. Mnapojadili pamoja maswali yaliyopo hapa chini, lenga kuweka wazi mtazamo wako binafsi unapopitia mawazo ya msingi ya kipengele hiki. Soma maswali yafuatayo kwa umakini, na utafute kuyajibu kwa kujenga majibu yako juu ya msingi wa fundisho la Biblia. 1. Orodhesha angalau aya tatu za Biblia zinazothibitisha kwamba maandiko yamevuviwa na Mungu, yaani “yamepuliziwa na Mungu,” kupitia nguvu na utendaji kazi wa Roho Mtakatifu. Tunamaanisha nini tunaposema kwamba Biblia ni kitabu cha kimungu na pia ni matokeo ya uandishi wa kibinadamu? Je, unalielewaje andiko la 2 Petro linalosema kwamba hakuna andiko lolote lipatalo kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu, bali waandishi “waliongozwa” na Roho Mtakatifu (taz. 2 Pet. 1:19-21)? 2. Nadharia ya Kiimla ni ipi, inaamini nini, na una maoni gani kuhusu kuaminika kwake? 3. Elezea Nadharia ya hisia ( Intuition ) au ya Asili ya uvuvio wa Biblia, na ni jinsi gani tunapaswa kuifasiri kulingana na kile ambacho Biblia yenyewe inajizungumzia? 4. Taja sifa za msingi za Nadharia ya Kuangaziwa ya uvuvio wa Biblia. Je, maandiko yanajibuje hoja ya karama za waandishi na uandishi wa kimungu wa Biblia? 5. Nadharia ya Viwango tofauti vya Uvuvio inahusianaje na mafundisho ya Biblia kuhusu asili ya Neno la Mungu? 6. Orodhesha dhana kuu zinazohusiana na Nadharia ya Uvuvio wa neno kwa neno au Uvuvio Kamili. Kwa nini nadharia hii, zaidi ya nyinginezo, inatupa jibu la wazi la uhusiano wa kimungu na binadamu katika asili na mamlaka ya Biblia? 7. Uhakiki wa kisasawaBiblia una lengo gani? Je, hili ni lengo linalowezekana? Elezea jibu lako. 8. Fanya muhtasari wa vipengele mbalimbali vya uhakiki wa Biblia ambavyo vinafuatilia mchakato wa upatikanaji wa Biblia kuanzia kwenye tukio la kimungu hadi nakala za maandiko tulizonazo sasa. Kuna tofauti gani kati ya uhakiki wa «juu» na uhakiki «wa chini»? Je, ni matatizo na manufaa gani yanayohusiana na taaluma hizi?
Sehemu ya 2
Maswali kwa wanafunzi na majibu
1
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker