Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
5 0 /
K U T A F S I R I B I B L I A
9. Kati ya njia zote tofauti za uhakiki wa Biblia, ni ipi unaamini inawapa wanafunzi waaminifu wa maandiko msaada bora na muhimu katika jitihada zao za kutafsiri Neno kwa usahihi? 10. Kwa nini tunapaswa kuwa na uhakika kwamba tafsiri ya maandiko tuliyo nayo ni ya kuaminiwa na kutegemeka, bila kujali mashaka makubwa yanayoonyeshwa na wasomi wengi leo kuhusu mamlaka na uvuvio wa Neno la Mungu?
Soma kiambatisho «Mtazamo wa Kristo kuhusu Biblia» cha Paul Enns ili kupata mtazamo muhimu juu ya njia ambayo Yesu wa Nazareti alitambua na kutumia maandiko ya Agano la Kale, na jinsi alivyotangulia kuuona ujio wa Agano Jipya kupitia mitume.
1
MUUNGANIKO
Asili ya Usomi wa Kisasa wa Kibiblia
Muhtasari wa Dhana Muhimu
Wingi wa mbinu za ufafanuzi wa Biblia (exegesis) zilizopo kwa sasa unachanganya na unaweza kumfanya mtafsiri ajaribiwe kujikita kwenye mbinu zaidi badala ya kuzingatia hatua muhimu za mchakato wa kuelewa. Pale ambapo wigo kamili wa tatizo unaonekana (pamoja na viwango vyake vya “kiontolojia”) kama hatua ya kuanzia, inawezekana kuainisha mbinu kulingana na kipengele muhususi cha tatizo kinachoshughulikiwa, na kuchagua mbinu inayofaa zaidi katika kila kesi. Kipengele cha kihistoria cha utafiti kinahusiana zaidi na uhusiano kati ya mpeleka ujumbe na ujumbe husika. Idadi kubwa ya mbinu maalumu zimetokana na eneo hili muhimu la utafiti. Utafiti wa usuli ya maandishi, yaani historia yake (Zeitgeschichte) huzingatia mazingira ya kihistoria ambamo maandishi yalitoka. Uhakiki wa muundo huunda dhana ya mapokeo ya mdomo yaliyotangulia maandishi yaliyoandikwa, kisha kujikita katika kutafiti mabadiliko yake kutoka katika muundo wa kabla ya fasihi hadi muundo wa fasihi. Uhakiki wa chanzo huchunguza uhusiano kati ya matini mahususi katika muktadha mpana wa kifasihi na utegemezi wa matini hayo kwa vyanzo vyake. Uhakiki wa uandishi unatokana na dhana kwamba waandishi wa vitabu vya Biblia walikuwa na ushawishi mkubwa juu ya muundo wa mwisho wa vitabu husika, na hivyo uhakiki huu huchanganua utunzi wa maandiko haya kwa kuzingatia mtazamo wa mwandishi wa mwisho wa kitabu. Uhakiki wa maandishi ni taaluma maalum na ya kiufundi inayolenga kurejesha kwa usahihi iwezekanavyo muundo asilia unaodhaniwa kuwa wa matini husika. Maswali ya uandishi, historia ya kitabu kimoja kimoja, na
page 314 6
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker