Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide
/ 6 9
K U T A F S I R I B I B L I A
I. Maana, dhumuni, vipengele, na faida za Mbinu ya Hatua Tatu ya kutafsiri Biblia.
Muhtasari wa kipengele cha 1 cha Video
A. Maana: “kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza ya andiko ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu.”
1. “Kuelewa maana iliyokusudiwa katika mazingira ya kwanza : Hatua ya kwanza inalenga kuelewa maandiko yalimaanisha nini katika muktadha wake wa asili.”
2
2. Ili tuweze kugundua kanuni za jumla za Kweli ya Neno: Hatua ya pili inalenga kupata kanuni za kibiblia katika maandiko hayo ambazo zinawahusu waamini leo.
3. Ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu binafsi ndani ya uhuru wa Roho Mtakatifu : hatua ya tatu ni kuhusianisha kanuni za Kweli ya Neno na maisha yetu binafsi katika nguvu za Roho Mtakatifu.
B. Dhumuni
1. Kujifunza mwandishi alimaanisha nini katika muktadha wa kwanza wa andiko.
2. Kutambua kanuni za kibiblia zinazotoa muhtasari wa maandiko na kutoa hekima ya Mungu na ufahamu ambao unawahusu watu wote na unaweza kutumika kwa wote.
3. Kubadili mitazamo na matendo yetu na kuyafanya maisha yetu yaendane na kweli zilizomo katika Neno la Mungu.
Made with FlippingBook - Online Brochure Maker