Kutafsiri Biblia: Capstone Module 5 Swahili Mentor Guide

7 0 /

K U T A F S I R I B I B L I A

C. Vipengele.

1. Inawiana na mbinu ya sarufi ya kihistoria : kutafuta maana ya maandiko katika mazingira yake ya asili kabla ya kutumia maana yake katika zama na mazingira tofauti.

2. Mbinu hii inatafuta maana ya wazi (dhahiri, isiyofichika) ya maandiko.

3. Mbinu hii inathibitisha ufunuo endelevu .

2

a. Biblia inaonyesha kwamba Mungu ameendelea kufunua maana na njia ya kusudi lake, ambalo lina kilele chake (yaani, “linahitimishwa”) katika Yesu Kristo, Ebr. 1:1-3.

b. Yesu yuko juu ya yote na anatimiza maana ya yote ambayo Mungu ameyasema tangu mwanzo (taz 1:14-18; Mt. 5:17-18; Yoh 5:39 40; Lk 24:27, 44-48).

4. Inathibitisha umoja wa maandiko .

a. Biblia ni kanoni moja (mkusanyiko, maktaba) ya maandiko, iliyoandikwa na mwandishi mmoja (2 Tim. 3:16-17; 2 Pet. 1:20-21).

b. Mada ya wazi ya maandiko ni Yesu Kristo na Ufalme wake, Mdo 28:23,31; Kol. 1:25-27; Efe. 3.3-11; Rum. 16.25-27.

Made with FlippingBook - Online Brochure Maker